24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

SIKUTAKA RONALDO ARUDI OLD TRAFFORD’

TURIN, ITALIA

MAMA wa Cristiano Ronaldo, Maria Dolores Aveiro, amekanusha taarifa kwamba, alimtaka staa huyo kurudi katika klabu ya zamani ya Manchester United mara baada ya kumalizana na Real Madrid.

Kuna baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari jijini Manchester, vilitoa taarifa kwamba mama wa mchezaji huyo anamtaka mwanaye kurudi viwanja vya Old Trafford katika klabu yake ya zamani ya Man United ikifikia hatua ya kumalizana na Madrid.

Kwa sasa mchezaji huyo tayari amejiunga na klabu ya Juventus, hivyo mama yake amefunguka kwa mara ya kwanza na kudai hakuwahi kusema lolote juu ya mchezaji huyo kurudi katika klabu yake ya zamani.

“Ni uongo kwamba niliwahi kusema kuwa nataka mwanangu arudi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United, kila siku nimekuwa nikifurahia maamuzi yake.

“Familia kwa ujumla tuna furaha kutokana na maamuzi yake, ninaamini mtoto wangu atafanya makubwa. Haya ni maisha yake mapya, alikuwa na furaha wakati yupo Real Madrid, lakini sasa ameamua kutafuta changamoto nyingine,” alisema mama wa staa huyo.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 33, ameondoka Real Madrid baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka tisa, huku akichukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mara nne pamoja na kuwa kinara wa mabao ndani ya klabu hiyo huku akiwa na jumla ya mabao 450 katika michezo 438 aliyocheza.

Wakati anakipiga katika klabu ya Man United, aliweza kuweka historia ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu na kutajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles