24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Siku ya Wanawake: Nauona mkono wa rais – Ado Shaibu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema, anauona ‘mkono’ wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuelekea uhuru wa habari nchini.

Amesema, kila tawala inacho cha kujivunia na kwamba, katika Awamu ya Rais Samia, miongoni mwa historia yake kama kiongozi wa nchini, ni kuitoa tasnia ya habari gizani.

Ado ametoa kauli hiyo leo Machi 8, 2023, ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwamba, Rais Samia amekuwa mfano bora kwa viongozi wanawake ndani na nje ya nchi.

Ado Shaibu.

“Unapozungumzia uongozi wa Rais Samia kama mwanamke, tunaweza kuona mifano mingi. Kipindi cha nyuma kidogo tulikuwa gizani; mnajua nyinyi wenyewe hali ilikuwaje?.

“Leo unapozungumzia mafanikio ya mchakato wa Mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari, ndani yake unaona msukumo mkubwa wa Rais Samia. Na katika hili, historia yake ndani ya nchi hii itaandikwa,” amesema Ado.

Amesema, Rais Samia amekuwa imara katika kuangalia haki za kila upande, ameitazama sekta ya habari kama kiongozi wan chi na akaona kuna tatizo kama ilivyokuwa katika demokrasia ya vyama vingi.

Na kwamba, hata baada ya kuona tatizo, amechukua hatua ‘haya yote ameyafanya kama kutafuta suluhu katika kila upande, namuona kama kiongozi mwanamke jasiri na anayeweza kutolewa mfano..

Hata hivyo, Ado amesisitiza kwamba haoni sababu hata moja kwa tasnia ya habari kuundiwa Baraza la Habari ambalo litasimamiwa na serikali.
Amesema, ndani ya tasnia ya habari kuna watu wenye weledi mkubwa na wenye uwezo wa kujisimamia.

“Kuna mifano katika hili, nakumbuka katika zile vurugu za gesi Mtwara. Ni weledi wa wanahabari pekee waliomaliza vurugu bila kutumia mtutu wala vitisho, kutokana na weledi wao, walikubaliana na kuandika tahariri ambayo ilizima kabisa vurugu Mtwara.

“Angalia kilichofanyika mwaka jana kwenye Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, Afrika nzima ilikuja Tanzania kusherehekea, wanahabari ndio waliopanga hili na atokeo yake Afrika nzima macho yao yalikuwa Tanzania. Acha wanahabari wajisimamie,” amesem Ado.

Mwanasiasa huyo kijana amesema, ikiwa waandishi wa Kenya wanalo baraza lao la habari lisiloingizwa mikono naserikali sawa na lile la Canada na hata Ghana, amehoji kwani Tanzania isichukue mkondo huo?

“Hoja ya kuwa na Baraza Huru la Habari inaungwa mkono hata na Jaji Mkuu, Profesa Ibrahimu Juma aliyewaambia waandishi wa habari, umuhimu wa kuwa na baraza lao la kitaaluma litakalosuluhisha kesi zote zinazohusiana na malalamiko kuhusu taaluma yao,” amesema Ado.

Pia amesema, Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18 na 19 zinatambua uhuru wa kujieleza, kutoa mawazo lakini hakuna sheria ya Bunge inayowapa nguvu waandishi kutambulika kisheria kama wanasheria, madaktari hivyo kukosa ulinzi kikatiba.

Anasema, waandishi wakitambulika kwa sheria ya Bunge, watasimamia masuala yao ya weledi na utendaji kazi na wanapokosea, kuadhibiana kupitia kamati za maadili kama ilivyo kwa tasnia nyingine nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles