Waandishi Wetu- mikoani, Dar na mikoa
VIONGOZI mbalimbali wametoa kauli nzito juu ya kushamiri kwa matukio ya ukatili wa kingono ambayo yamezidi kushamiri siku hadi siku
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema matukio ya ukatili wa kingono yanayoendelea kutokea kwa kasi nchini ambayo wanayofanyiwa wanawake na watoto wa kike, ni sawa na uhujumu uchumi.
Alisema kuendelea kushamiri kwa matukio hayo, ni kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kuhakikisha inapambana na matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo kufikia usawa wa kijinsia.
Samia alisema hayo jana, wakati akizungumza na na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa maazimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yalifanyika mkoani hapa.
Alisema matukio hayo, yamekuwa yakiwahathiri watendewa, bali waathirika wengine ni familia, jamii na taifa kwa ujumla, kutokana na idadi kubwa ya watendewa kuwa ndiyo wazalishaji wakubwa.
Alisema kumekuwepo na ongezeko la matukio hayo kutoka ambayo uripotiwa kwenye vituo vya polisi, kutoka matukio 31,996 mwaka 2016 hadi matukio 43,487.
Alisema ili vitendo hivyo viweze kupungua kama siyo kuisha kabisa, lazima jamii yote kwa ujumla iweze kupambana kupiga vita matukio haya ikiwa pamoja na wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
“Hii hali ni mbaya, taifa letu linaelekea kwenye hali mbaya, kila mmoja wetu achukue nafasi yake kuhakikisha anamlinda mtoto wake na mtoto wa jirani, kila mmoja apambane na vitendo hivyo, serikali peke yake haiwezi lazima kila mmoja apige vita,” alisema Samia.
Alisema inaendelea kutekeleza maazimio ya mkutano wa wanawake Beigin China uliofanyika mwaka 1995, ambapo katika upande wa usawa wa kijinsia kwenye elimu na mafunzo serikali inatoa elimu bure shule za msingi na sekondari.
Alisema utekelezaji wa sera hiyo ya elimu bure, itaondoa ubaguzi wa kielimu uliokuwepo kati ya mtoto wan a kiume, ambapo alisema serikali itawachukulia hatua kali wale wote ambao wanaowakataza watoto kwenda shule.
Alisema Serikali imekuwa ikiwawezesha wanawake kiuchumi, kupitia halmashauri kwa kuwapatia mikopo kupitia makusanyo ya mapato ya ndani asilimia 10, ambapo zaidi ya bilioni 9.7 zimetolewa kwa vikundi 14,870.
Katika kupunguza umaskini kwa wanawake, Makamu wa Rais alisema kuwa serikali ilianzisha mpango wa kunusuru kaya Maskini awamu ya tatu (TASAF III) ambapo asilimia kubwa ya walioko kwenye mpango huo ni wanawake.
Alisema serikali imeendelea kuwapa nafasibalimbali wanawake katika siasa na nafasi za uongozi, huku akiwasisitiza wanawake nchini kutumia fursa ya uchaguzi mkuu mwaka huu katika kuchukua fomu kugombea udiwani na ubunge.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa, Zlatan Milisic, aliipongeza Serikali kuwawezesha wanawake kwenye nyanja za uongozi na uamuzi.
Alisema Tanzania imetia saini makubaliano ya Jukwaa la Beijing pamoja na sheria nyingine za dunia ambazo zinahamasisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake na wasichana.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema kuwa ajenda ya usawa na jinsia na uwezeshaji siyo ya wanawake tu bali ni watu wote wakiwemo wanaume.
Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Chama cha wafanyabishara Wanawake Tanzania (TWCC), aliwataka wanawake nchini kutumia maazimisho hayo katika kujitadhimini walipo na kuweka mikakati ya kuboresha mbinu za kufikia malengo ya mafanikio kwa baadaye.
Ofisa Habari na mahusiano Shirika la Word Vision Agness John, alisema kuwa wameendelea kuwasadia wanawake kupitia vikundi vya ujasliamali katika ili kuondokana na matukio ya ukandamizwaji katika jamii na familia kwa jumla.
MAKONDA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema kuazia leo (jana), atawashughulikia kikamilifu wanaume wenye tabia ya kuwaonea wanawake kwa kuwapiga hadi kuwaharibu mwonekano wa sura, macho,kuwavunja meno au taya na kusababisha baadhi yao kupata ulemavu wa kudumu jambo ambalo ni kinyume na Sheria.
Alisema mwanamke yoyote atakayeshushiwa kipigo na mwanaume kuanzia sasa atoe taarifa kupitia simu ya mkononi.
Alisema baadhi ya wanaume wamekuwa na tabia ya kuwadharau wanawake kutokana kutokuwa na elimu au kipato jambo ambalo alisema hawezi kulivumilia katika mkoa huo.
“Kiongezwe kipengele cha kutaka asilimia asilimia 40 ya mshahara wa mwanaume apatiwe mwanamke asiefanya kazi kwa ajili ya shughuli za familia ili kumsaidia kumjengea uwezo,” alisema Makonda.
CUF
Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha Wananchi (CUF),imeiomba Serikali kuanzisha sera madhubuti zitakazoamuru kila shule kuwe na utaratibu wa kugawa taulo za kike bure ili kuchochea ufaulu kwa wanafunzi wa kike.
Katibu wa Jumuiya hiyo, Anna Paul alisema, zipo sababu nyingi zinazochangia kushuka elimu kwa watoto wa kike, ikiwamo mazingira ya kimaumbile wanayokabiliana nayo.
Alisema ili kuwajengea umakini wakiwa darasani, ni vema kukawekwa utaratibu maalum utakaompa uhakika mwanafunzi huyo wakuwa safi na salama pindi anapokuwa kwenye hedhi.
JOKETI
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,Joketi Mwegilo aliwataka wanawake kujiamini, kujituma na kujenga familia bora kwa kufata misingi ambayo itawasaidia kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazowakabili pindi wanapokumbana nazo.
Alisema wanawake wanatakiwa kuacha kujibweteka na kuchukulia changamoto kama chachu ya maendeleo katika katika nyazifa zao na jamii kiujumla.
Alisema wanawake wanapokuwa kwenye uongozi au utendaji hawatakiwi kuogopa changamoto wanatakiwa kuzikabili.
“Wanawake wanatakiwi kutokujiweke nyuma wanatakiwa kujishughulisha na kujikita kwenye biashara jiwezeshe na kujiunga kwenye vikundi mbali mbali vitakavyo kusaidia kupata mikopo,”alisema
Alisema alipoteuliwa kwenye nafasi ya kuwa mkuu wa wilaya wapo watu wakisema kuwa mdogo awezi kufanya kazi katika ngazi hii.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kisarawe, Eve Station alisema ni wakati wa mwanamke kuishi kwenye ndoto na kipaji chako sio, unapoolewa tu unakatishwa kipaji chako tuinuke na tulete maendeleo kwenye nchi yetu.
JKCI
Ofisa Lishe wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Maria Samlongo amewataka wanawake kuzingatia lishe bora katika familia zao ili kuepukana na magonjwa ya moyo.
Alisema lishe bora kama sehemu ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ikiwemo magonjwa ya moyo.
“JKCI tunamchukulia mwanamke kama sehemu muhimu katika magonjwa ya moyo, anatumika kununua chakula,kukipika au kuandaa mpaka kinafika mezani,”alisema.
TANGA
Huko mkoani Tanga, wametakiwa kuchangimkia fursa ya kauli mbiu ya awamu ya tano kuelekea uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na vikubwa ili kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zinazowazunguka.
Hayo yalisemwa jana na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga, Specioza Owure.
Alisema kina mama wasilaze damu kwa kuhakikisha wanachangamkia fursa, ikiwemo kujiunga kwenye vikundi na kuanzisha viwanda ambavyo vitakuwa chachu kubwa ya kufikia mafanikio na kuweza kuwainua kiuchumi.
KATAVI
Taarifa kutoka mkoani Katavi, zinasema wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa, wametowa msaada kwa mahabusu wa kike walioko gereza Mpanda, ikiwemo mashine ya kisasa ya kunyolea nyele itakayosaidia usalama wao.
Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba ya wanawake wa chama hicho, Makamu Mwenyekiti wa TUGHE, Mary Buberlwa alisema wameona ni vema kile kidogo walichonacho waweze kuwasaidia wenzao waliko mahabusu ili kuwapa moyo na nguvu wasijifikirie vibaya kuwemo kuwa mahabusu