24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Siku ya Mashujaa yaadhimishwa vingine

AUGUSTINO LACHUO (TUDARCO) Na JOHANES RESPICHIUS

-DAR ES SALAAM

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jana liliadhimisha Siku ya Mashujaa kwa    kufanya shughuli za  jamii tofauti na ilivyo desturi yake ya kuandaa gwaride, kuweka mikuki, ngao na mashada ya maua kwenye mnara wa mashujaa wa Mnazi Mmoja,  Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo ambayo hufanyika Julai 25 ya kila mwaka, jana pia yaliadhimishwa kwa wanajeshi kupima afya zao, kuchangia damu salama huku baadhi yao wakifanya usafi kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza katika viwanja vya Mnaz Mmoja Dar es Salaam baada ya kukagua mabanda ya kutoa huduma ya kupima afya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Florens Turuka, alisema Serikali imeamua kuadhimisha siku hiyo kwa mtindo huo  kupunguza gharama.

“Tumezoea katika siku kama ya leo (jana) majeshi ya ulinzi huwa yanafanya shughuli maalum ya kuweka mashada ya maua na ngao katika minara ya mashujaa katika sehemu mbalimbali za nchi.

“Kwa mwaka huu Serikali imeamua isifanye hivyo kwa sababu ya gharama kubwa bali tufanye kwa namna inavyoweza kusaidia kuonyesha ni jinsi gani jeshi limekuwa likienzi mashujaa wetu na katika eneo hili la Mnazi Mmoja watatoa huduma ya afya,” alisema DK Turuka.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, alisema wameamua kuadhimisha siku hiyo tofauti  kupunguza gharama na kusaidia wananchi kupima na kuangalia afya zao.

“Zamu hii tumeamua kuwashirikisha wananchi hasa katika suala la kupima na kuangalia afya zao, kufanya usafi   na wadau kushiriki kuchangia damu   kuwasaidia watu wenye uhitaji   hospitalini,” alisema CDF Mabeyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles