28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

SIKU 100 MADARAKANI Rais: Rodrigo Duterte aua watu 3,700

rodrigo-duterte* Avunja uhusiano wa kijeshi na Marekani

VITA inayoendeshwa na Rais wa Philippines Rodrigo Duterte dhidi ya wauzaji na watumiaji wa mihadarati machoni mwa jumuiya ya kimataifa imefikia pabaya kutokana na idadi kubwa ya vifo ndani ya miezi mitatu tu akiwa madarakani, kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi ulioendeshwa na televisheni ya Kiarabu ya Al-Jazeera.

Aidha, kutokana na kile kinachoonekana kukerwa na shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu zikiongozwa na mshirika mkubwa wa taifa hilo, Marekani, Kiongozi huyo makeke amechukua uamuzi wa usiotarajiwa wa kuvunja ushirikiano wa miaka 65 wa kijeshi na taifa hilo.

Akiongozwa na hisia na mihemko Duterte, ambaye kitaaluma ni mwanasheria amechukua uamuzi huo huku akiiamuru Marekani kuondoa majeshi yake kutoka pwani ya nchi hiyo.

Mbali ya msimamo wake, matamshi yake daima huzua utata na kutengeneza vichwa vya habari duniani.

Anakumbukwa kumtusi Rais wa Marekani Barack Obama, akimuita mwana wa kahaba na karibuni kabisa amezua utata kwa kujilinganisha na dikteta wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler.

Siku za mwanzo madarakani alitangaza hadharani kuwa nchi yake, ambayo imekuwa mshirika mkuu wa Marekani, haitategemea Washington.

Alishamtusi pia Papa Francis, kiongozi wa Kanisa la Katoliki Duniani, ambalo lina wafuasi wengi zaidi nchini humo. Pia alimtusi Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry kwa kumuita ‘mwendawazimu’

Na alimwelezea balozi wa Marekani nchini humo kuwa shoga na mwana wa kahaba.

Alifanya mzaha na kusema kwamba alipokuwa meya angekuwa mtu wa kwanza kumbaka mmisionari kutoka Australia aliyeuawa wakati wa ghasia gerezani.

Wakati alipokutana ana kwa ana na anayeaminika kuwa kinara wa unga nchini humo, Peter Lim, baba huyo wa watoto wanne katika mkutano huo usio wa kawaida alimtisha mfanyabiashara huyo akimtahadharisha aachane na biashara hiyo haramu vinginevyo apotee duniani.

“Nitakuua… Nitakuangamiza kabisa,” Rais Duterte ananukuliwa akisema wakati wa mkutano huo na mshukiwa huyo Julai mwaka huu.

Na katika mdahalo wa televisheni alitishia kuwaua watoto wake iwapo watatumia mihadarati.

Yote hayo yamemuongezea sifa miongoni mwa wengi nchini Philippines kama mtu anayeweza kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha mambo muhimu yanatekelezwa.

Na hilo linakumbushia wakati akiwa meya wa mji wa Davao, alipoubadili na kuwa moja ya miji salama zaidi nchini humo

Amekuwa akilinganishwa na mgombea wa urais wa Marekani Donald Trump, lakini alikataa kufananishwa naye, akisema mgombea huyo wa chama cha Republican hakubali maoni ya wengine tofauti na yeye.

Lakini kelele dhidi ya machinjo makubwa yanayoendelea dhidi ya watumiaji wa dawa za kulevya mikononi mwa wanamgambo katili na polisi imemzidisha kiburi.

Vita yake kichaa dhidi ya mihadarati hadi sasa imeua watu zaidi ya 3,700 chini ya miezi mitatu, kwa mujibu ya ripoti ya Al Jazeera.

Duterte aliamuru mapambano dhidi ya mihadarati kutimiza ahadi yake ya wakati wa kampeni na kuchochea umwagaji mkubwa wa damu –ikiwa ni sawa na Wafilipino 36 kufa kila siku katika siku zake 100 za kwanza madarakani.

Kihoro cha kutisha kinaweza kuonekana katika picha mbalimbali zilizopo mitandaoni.

Vita ya Duterte dhidi ya mihadarati inakuja baada ya Wafilipino milioni 3.7 kuwa tegemezi wa dawa za kulevya aina ya methamphetamine, ambazo hujulikana nchini humo kama shabu.

Pia amewaruhusu raia kuchukua sheria mikononi kuwasaidia polisi na vikosi vya siri vya mauaji katika kuangamiza watuhumiwa.

Gazeti la The Huffington Post linaripoti kuwa mauaji huendeshwa na wanamgambo wenye silaha wanaopanda pikipiki au askari polisi na au vikosi visivyo rasmi vya siri vya mauaji.

Moja ya kesi ya kusikitisha ni kumhusu msichana mdogo wa umri wa miaka mitano aliyeuawa na mtu mwenye silaha aliyeachia risasi wakati babu na baba yake na mtoto waliokuwa wakivuta shabu wakipigwa risasi na kuuawa mikonini mwa polisi.

Hofu ya kuuawa imechochea wauzaji wengi kujisalimisha wenyewe polisi huku watu zaidi ya 26,000 wakikamatwa na makumi kwa maelfu wakijisalimisha kwa mamlaka husika.

Hilo limesababisha hali mbaya isiyoelezeka magerezani na vituo 44 vya kubadili tabia nchini humo.

Mbinu ya hofu imeshuhudia umaarufu wa Duterte ukipanda huku utafiti wa Vituo vya Hali ya Kijamii uliofanyika mwishoni mwa Septemba ukionesha Wafilipino wanane kati ya 19 wanaridhishwa na kampeni zake dhidi ya mihadarati wauzaji na watumiaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles