28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Sikonge wazindua kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki

Na Allan Vicent, Tabora

Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora imezindua mradi wa kiwanda cha kati cha kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki ambao hadi kukamilika kwake utagharimu Sh milioni 757.5.

Akitoa taarifa ya mradi huo mwishoni ma wiki Ofisa Mipango wa halmashauri hiyo, Gadi Mwatebela alisema mradi huo unatekelezwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mfuko wa Misitu Tanzania.

Alisema ujenzi wa miundombinu ya mradi huo ambao utekelezaji wake ulianza Oktoba 6, 2020 inatarajiwa kukamilika Agosti 8, mwaka huu ambapo inahusisha ujenzi wa jengo la kiwanda, uzio na kitako cha tanki la kuhifadhia maji.

Alibainisha kuwa mradi huo unatekelezwa kwa awamu 2 ambapo awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa kiwanda na awamu ya pili ni ununuzi, usafirishaji na usimikaji mitambo ambapo utagharimu Sh milioni 757.5. 

Alifafanua kuwa kati ya fedha hizo milioni 719.7 ni mchango wa serikali kuu namilioni 37.8 ni mchango wa halmashauri na fedha zilizokwisha pokelewa hadi sasa ni milioni 729.07 za Mfuko wa Misitu Tanzania na Sh 9.3 za halmashauri.

Mwatebela alibainisha kuwa kati ya Sh milioni 719.7 zilizotolewa na Mfuko wa Misitu milioni 462.5 ni za ujenzi wa kiwanda na Sh milioni 257.1 ni za ununuzi, usafirishaji na usimikaji wa mitambo.

Alieleza kuwa hadi sasa wameshatumia Sh milioni 433 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda ambapo kwa sasa wapo katika hatua ya umaliziaji, kazi za ujenzi wa uzio, mashimo ya majitaka na kitako cha tanki la maji zinaendelea.

Alisema kukamilika kwa mradi huo wenye uwezo wa kuchakata tani 8 za mazao ya nyuki kwa siku kutakuwa na manufaa makubwa kwa wafuga nyuki wa Sikonge kwani watapa soko la uhakika la asali, kuongeza kipato na kupunguza umaskini.

Akizindua kiwanda hicho Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Lt Josephine Paul Mwambashi alipongeza kazi nzuri iliyofanywa na halmashauri hiyo na kusisitiza umuhimu wa kutunza taarifa za kila kinachofanyika na gharama zilizotumika katika kila hatua ya mradi.

Aidha aliwataka Wasimamizi wa miradi yote inayotekelezwa na serikali kuhakikisha viongozi wa ngazi za chini na jamii kwa ujumla wanashirikishwa ipasavyo ili kujua kinachofanywa na serikali yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles