30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

SIDO YAWAFUNDA WAJASIRIAMALI KUANZISHA VIWANDA

Hadija omary, Lindi

Jumla ya Wajasiriamali 36 kutoka wilaya za Ruangwa, Kilwa, Nachingwea, Lindi na Lindi Manispaa wamenufaika na elimu ya uanzishaji wa viwanda katika maeneo yao yaliyotolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).

Meneja wa Sido Mkoa wa Lindi, Mwita Kasisi amesema hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa Sera ya Taifa kuelekea kwenye uchumi wa kati na viwanda.

Akizindua mafunzo hayo juzi, meneja huyo amesema: “Ili kufikia malengo hayo ni wajibu wa taasisi mbalimbali za umma ikiwemo Sido kuwaandaa wananchi kushiriki kwenye mpango huo kwa kuwapa maarifa na ujuzi utakaowasaidia kuanzisha viwanda vitakavyoendana na upatikanaji wa bidhaa na maligahafi kulingana na mazingira.”

Akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga amezitaka taasisi zinazotoa elimu kwa umma kutokana na matokeo ya elimu wanayoitoa ili kujua mafanikio na changamoto na kuzifanyia kazi.

“Nawasihi wajasiriamali mliopata mafunzo haya, mjitahidi kuwa wanyenyekevu kwa wateja ili mkuze biashara zenu na kuleta tija kwa taifa,” amesema.

Kwa upande wake mjasiriamali aliyepata mafunzo hayo, Isaac Daniel amesema mafunzo waliyopatiwa washiriki hao ni namna ya utengezaji wa pilipili (mango pickle), tomato sauce, Jam, juisi ya embe, wine za matunda mbalimbali, unga wa lishe  na mengineyo ambayo yatawasaidia kujiendesha kibiashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles