22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

SIASA ZAMRUDISHA JAGUAR KWA MUNGU

NAIROBI, KENYA


MKALI wa muziki nchini Kenya, Charles Njagua maarufu kwa jina la Jaguar, ameamua kumrudia Mungu wake mara baada ya kuona ugumu kwenye kampeni za kuwania ubunge kupitia chama chake.

Wiki iliyopita msanii huyo alitajwa kuwa amepita katika kura za maoni dhidi ya mpinzani wake, Maina Kamanda, lakini baadaye taarifa ikatoka kwamba kulikuwa na makosa hivyo matokeo yalibadilishwa na Maina akatangazwa mshindi huku akimwacha Jaguar akibaki kulalamika.

Kutokana na hali hiyo, Jaguar alionekana akidondosha machozi mbele ya wananchi kwa kuwa aliamini tayari amemaliza kila kitu, lakini watu hao walimshauri amuunge mkono mshindi na wafanye kazi pamoja.

Hali hiyo imemfanya msanii huyo amrudie Mungu wake kwa kufanya maombi ya mara kwa mara huku akikutana na wachungaji mbalimbali akiwamo Margaret Kenyatta.

“Ninaamini Mungu ndio kila kitu kwangu, hata kama kuna mchezo unachezeka, ila ninaamini malipo yake yako hapa hapa, kikubwa ninachokifanya ni kumshitakia Mungu wangu,” alisema Jaguar.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,215FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles