26 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

SHULE YA FOUNTAIN GATE YAONGOZA MATOKEO YA DAR ES SALAAM

 

 

Na Mwandishi Wetu

SHULE ya Msingi Fountain Gate Academy ya Tabata, imefanikiwa kuwa ya kwanza katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu kwa shule zilizopo Dar es Salaam zikiwa na watahiniwa chini ya 40.

 

 

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa shule hiyo, Japhet Makau, alisema matokeo yaliyotangazwa juzi na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) yanaonyesha shule hiyo imeongoza Dar es Salaam yenye shule 152 na imeongoza Wilaya ya Ilala iliyokuwa na shule 22.

 

Pia alisema shule yake iliyokuwa na watahiniwa 36, imepata wastani wa alama 220 ambayo ni mafanikio makubwa.

 

Makau alisema mafanikio hayo yametokana na bidii ya walimu na kuwaandaa vizuri wanafunzi hao kwa ajili ya mitihani ya kitaifa.

“Tuliwaaminisha wanafunzi wetu kuwa kwamba wao ni washindi na hakuna kitu kipya kitakachokuja zaidi ya yale waliyofundishwa, tunaona fahari kwa mafanikio haya,” alisema.

Makau alisema shule hiyo ilianzishwa miaka 10 iliyopita na imeshatoa wanafunzi wa darasa la saba mara nne na imeweza kufanya vizuri katika matokeo yao ya mitihani yote ya kitaifa.

Alitoa mfano kuwa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka juzi, shule hiyo ilishika nafasi ya tano kati ya shule zaidi 500 zilizopo Dar es Salaam.

Alisema shule hiyo inawafundisha watoto kuwa na upendo hasa kwa masikini na yatima na kuwaandaa kuwa viongozi wa Taifa la kesho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles