SHULE 35 KUSHIRIKI MASHINDANO YA UMITASHUMTA MOSHI

0
1010

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Shule 35 za msingi za serikali na binafsi, zinatarajiwa kushiriki Mashindano ya Michezo ya Wanafunzi wa Shule za Msingi nchini (Umitashumta) katika Manispaa ya Moshi.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo ngazi ya kata katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwereni, Mwalimu wa michezo wa manispaa hiyo, Laurence Temba, amesema lengo la mashindano hayo ni kuyafuta vipaji.

Amesema pia lengo ni kutafuta wanafunzi 100  watakaowakilisha Mkoa wa Kilimanjaro, kwenye mashindano hayo ngazi za taifa ambayo yatafanyika jijini Mwanza.

“Katika mashindano hayo, wanafunzi watashiriki michezo mbalimbali ikiwemo, mpira wa miguu, mpira wa pete kwa wasichana, kukimbia mbio ndefu, kuruka chini, kurusha kitufe,  kisahani na michezo wa mpira wa kengele kwa wanafunzi kwenye ulemavu,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here