24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Shirika lahimiza ulaji wa mbogamboga

Na JANETH MUSHI – ARUSHA

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Agri Thamani Foundation, limeingia makubaliano na kituo cha utafiti wa mbogamboga na matunda cha kimataifa cha World Vegetable Center, kuhamasisha uzalishaji na ulaji wa mboga kuimarisha lishe na kutokomeza udumavu na utapiamlo.

Agri Thamani iliyojikita kutokomeza udumavu na utapiamlo, imeingia mkataba huo wa miaka mitano, ambao kwa kuanzia unatarajiwa kutekelezwa katika mikoa saba.

Akizungumza jana jijini Arusha wakati wa kusaini mkataba wa makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Agri Thamani, Neema Lugangira alisema makubaliano hayo yapo katika maeneo saba na lengo likiwa ni kutokomeza udumavu na utapiamlo.

Neema alisema wataanza na mikoa ya Kagera, Geita, Dodoma, Tabora, Kigoma na Tanga.

 Alisema katika mikoa hiyo, watapeleka elimu lishe na kuanzisha bustani za mfano kwenye shule za msingi na sekondari za Serikali.

Neema alisema wameamua kuungana ili kuimarisha jitihada za serikali na wadau kwani serikali imeshaweka mfumo mzuri na ina mpango jumuishi wa kuboresha lishe nchini ambao unajumuisha sekta zote muhimu.

“Hii mikoa tumeichagua kimkakati kwa sababu ni mikoa ambayo inaongoza kwa changamoto ya udumavu, lakini ni mikoa ambayo ulaji wa mboga na matunda uko chini ndo maana tunaanza nayo,” alisema Neema.

Alisema wataanzisha bustani za mfano kwenye shule, kaya zenye watoto chini ya umri wa miaka mitano na wenye uhitaji mkubwa wa lishe, zoezi litakaloanza mwezi huu.

Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa kituo hicho, Dk. Gabriel Rugalema alitaja miongoni mwa maeneo waliyoingia makubaliano ni pamoja na kueneza elimu ya kilimo na lishe kwa jamii na kuweka msukumo wa kuhamasisha ulaji wa mbogamboga na matunda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles