25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Shirika la Taifa la Uvuvi laja na mikakati mipya

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Taifa la Uvuvi (TAFICO), limeanza kujipanga upya ili kuhakikisha sekta ya uvuvi inashika kasi na kutoa ajira zaidi.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari mwishoni wa wiki waliotembelea makao makuu ya shirika hilo, Kigamboni, Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mkuu wa TAFICO, Esther Mulilya alisema kurejea kwa shirika hilo kutasaidia mno Watanzania kufaidi rasimali za uvuvi katika ukanda wa uchumi wa bahari kuu ambao haujafikiwa muda mrefu.

“Tumejipanga vizuri kurudisha shirika letu ili litimize majukumu yake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, tunagetemea sasa tutafikia kwenye uvuvi kwenye ukanda wa bahari kuu ambako hatujafika miaka mingi,”alisema.

Alisema ili kufika kwenye ukanda huo, wameweka mikakati mikuu mitatu ambayo moja wapo, ni ununuzi wa meli mbili kubwa za uvuvi ambazo zitatumika kuvua samaki ukanda wa bahari kuu.

“Tumejiwekea mikakati mikuu mitatu, moja wapo ni kununua meli kubwa za uvuvi za kitaifa ambazo zitafanya kazi kwenye ukanda huu ambao una utajiri mkubwa wa samaki… hii ni njia nzuri ya Serikali kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya uvuvi, tunategemea kupokea meli ya kwanza Juni, mwakani ambayo itatumia uvuvi wa mishipi.

Alisema meli hiyo itakuwa na urefu wa mita 200, ina nguvu ya kukaa baharini kwa siku 30 bila kurudi nchi kavu kutokana na kuwa na mahitaji yote ya msingi kwa watu watakaokuwamo.

“Meli hii itakuwa na injini kubwa, mishipi yenye uwezo wa kuwanana ndoano 500 na chambo chake ni samaki aina ya vibua ambao ni karibu tani nne hivii kwa siku zote 30 wavuvi wanapokuwa majini. Tunapenda vibua hawa tuwanunue kwa wavuvi wetu ili kuwaunga mkono na kukuza uchumi… katika eneo hili tungependa kuona makubwa makubwa ya wavuvi yanaungana kwa ajili ya kutuuzia samaki pindi tutakaopoanza kazi rasmi. “Tunataka tuwafikie wenzetu Japan ambao ndiyo vinara wa uvuvi kwenye ukanda

kama huu, tunaamini malengo yetu haya yatatimia kutokana na mipango kazi ambayo tumejiwekea wenyewe,”alisema.

Alisema miradi mingine ambayo wanaifanyia kazi, ni uzalishaji wa virafanga vya samaki na kuchakata samaki.

“Tumedhamiria kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki, tumeomba wizarani fedha ambazo zitatusaidia utekelezaji wa miradi hii yote ili iweze kufanikiwa,”alisema.

Alisema katika mipango yao, wamelenga zaidi soko la feri, kuhakikisha wanasambaza barafu ambayo watakuwa wanazalisha, kuzalisha samaki wafugwao, ufugaji wa kutumia vizimba pamoja na ufugajiwa samaki wa mabwawa.

Kuhusu ajira, alisema meli ya kwanza itazalisha ajira 15,000, wafanyakazi ndani 60, mama lishe watapa nafasi ya kuuza vyakula kwa sababu kutakuwapo na watu wengi.

Kwa upande wa changamoto, alisema kuna uchakavu mkubwa wa miundombinu ambayo ilikaa miaka 22 bila kufanya kazi ambayo baada ya tathimini iliyofanyika zinahitaji Sh milioni 644 kwa ajili ya ukarabati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles