25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Shirika la SATF latoa msaada wa Sh milioni 50 kuimarisha utendaji

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Shirika la Social Action Fund (SATF) linalojihusisha na kuwawezesha kielimu watoto walio katika mazingira magumu limekabidhi vitendea kazi vyenye thamani ya Sh milioni 51 zikiwemo kompyuta 18, ili kuimarisha utendaji kazi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Social Action Fund (SATF) linalojiusisha kusaidia watoto walio katika mazingira magumu, Beatrice Mgaya (kushoto) akimkabidhi kompyuta na vifaa kuunganishia mtandao,  Sista Suzana Misonji wa Kituo cha St. Maria Goreth kilichopo Bukoba mkoani Kagera wakati wa  kikao cha mpango kazi na wadau watekelezaji miradi ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu (implementing partners) uliofanyika mkoani Morogoro jana. Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Tamisemi, Dk. Johaness Balige na Meneja wa Miradi wa SATF, Nelson Rugambwa (kulia).

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Mei 28, 2021, mjini Morogoro, Meneja miradi wa shirika hilo, Nelson Rugambwa amesema vifaa hivyo vitasaidia katika utunzaji wa taarifa.

“Tumekabidhi vifaa hivi ikiwa ni pamoja na kompyuta 18 na vifaa vya kuunganishia mtandao vyenye thamani ya Sh milioni 51 kwa wadau watekelezaji (implementing Partners).

“Vifaa hivi vitasaidia katika utunzaji wa taarifa na kurahisisha mawasiliano ya kati yao na shirika, kwani tumeona katika kuboresha huduma zetu tuwapatie vitendea kazi wadau wetu ili kuwaondolea changamoto mbalimbali zilizokuwa zilizokuwa zikiwakwamisha katika utendaji wa kazi wao.

“Kwa sasa kazi zitakuwa rahisi sana maana watakuwa na kanzi data ya kutunza taarifa za miradi yao pamoja na kuwa na mawasiliano ya mtandao ya moja kwa moja na wasimamizi wa SATF na kufanya mawasiliano pasipo kulazimika kukutana moja kwa moja,” amesema Rugambwa.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa (SATF), Beatrice Mgaya, mara baada ya kuwakabidhi wadau watekelezaji (implementing partners) kompyuta 18 na vifaa vya kuunganishia mtandao vyenye thamani ya Sh milioni 51 amewataka kufanya kazi kwa weledi na uaminifu.

“Tumetoa vifaa hivi kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi, hivyo tufanye kazi kwa kujitolea ili kusadia jamii hasa watoto tuwawezeshe kupata elimu kutokana na changamoto zinazowakabili za ukatili, unyanyasaji, mazingira magumu na umasikini wa familia zao,” amesema.  

Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa wawakilishi wa vituo mbalimbali hapa nchini.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Social Action Fund (SATF) linalojiusisha kusaidia kielimu watoto walio katika mazingira magumu, Beatrice Mgaya (kushoto) akimkabidhi kompyuta na vifaa kuunganishia mtandao,  Afisa Mradi wa Kituo cha CCT Kibondo, Sengiyumvua Bisaga  wakati wa  kikao cha mpango kazi na wadau watekelezaji miradi ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu (implementing partners) uliofanyika mkoani Morogoro jana. Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Tamisemi Dk. Johaness Balige na Meneja wa Miradi wa SATF, Nelson Rugambwa (kulia).
 Afisa Mtendji Mkuu wa Shirika la Social Action Fund (SATF) linalojiusisha kusaidia watoto walio katika mazingira magumu, Beatrice Mgaya, akizungumza na wadau watekelezaji miradi ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu (implementing partners) wakati wa  kikao cha mpango kazi uliofanyika mkoani Morogoro jana.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles