24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Shirika la Posta latakiwa kwenda na kasi ya Teknolojia

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

NAIBU Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Kundo Mathew amezindua duka la Posta Mtandaoni (Posta Online Shop) ambalo litawawezesha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kununua na kuuza bidhaa zao kwa njia ya mtandao huku  akilitaka Shirika la Posta kujipanga kuteka soko la biashara mtandaoni kwani wanamatawi 350 nchini.

Akizungumza leo, Jumatano Septemba 6, jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa duka hilo ulioenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Posta Duniani, Naibu Waziri huyo amewaomba Watanzania kutumia huduma za Shirika hilo kwani kwa sasa zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.

Naibu Waziri huyo ambaye alimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Ashatu Kijaji amesema shirika hilo ndilo lenye mtandao mkubwa hivyo wanatakiwa kujipanga kwani soko la biashara mtandao lipo mikononi mwao.

“Ndani ya nchi tuna matawi 350, hivyo kama watajipanga katika biashara ya mitandaoni soko lipo mikononi mwao tunatakiwa kuwa wabunifu kutoka na teknolojia tuliyonayo,” amesema.

Mathew amesema uzinduzi wa duka hilo ni matokeo ya Maendeleo ya Teknolojia pia inakuja kutatua changamoto ya ugonjwa wa UVIKO 19.

Amesema duka hilo la posta mtandao litarahisishia wananchi waliopo maeneo ya pembezoni kupata huduma kwa haraka na kwa urahisi ambapo pia italeta tija na kuongeza kipato kwa wananchi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Dk. Zainabu Chaula ameeleza kuwa kazi ya wizara ni kuweka miundombinu itakayoiwezesha nchi kwenda kwenye Tanzania ya kidigital na kuwaomba wananchi kutumia huduma za posta kwani ni salama.

“Nafurahi kuona tuna mafanikio umoja ni nguvu  na ndio ambao utatuvusha kwani sisi tunatembea katika umoja,”amesema.

Naye, Kaimu Posta Masta Mkuu,Macrice Mbado  amesema kutokana na badiliko makubwa ya Teknolojia  ambayo yanaenda kwa kasi kubwa dunia shirika la posta limekuwa  likifanya  mageuzi na maboresho katika  utoaji wa huduma zake  ili kuendana na sera za Umoja wa mashirika ya posta duniani.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Jabir Bakari,amesema sekta ya posta imepita katika changamoto nyingi ambapo amedai TCRA imetoa leseni 119 katika sekta ya Posta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles