22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

SHIRIKA LA POSTA LAKUSANYA MADENI YA BIL. 7/6/-

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

SHIRIKA la Posta Tanzania (TPC), limefanikiwa kukusanya madeni ya muda mrefu kutoka kwa taasisi za Serikali, mashirika ya umma na sekta binafsi kiasi cha Sh bilioni 7.6.

Hayo yalisemwa juzi mjini hapa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Shirika, ambapo alisema makusanyo hayo ni kati ya jumla ya Sh bilioni 12 ambazo shirika hilo linadai wateja wake kuanzia mwaka 2011 hadi Juni mwaka huu.

“Hakikisheni mnamalizia makusanyo ya deni lililobaki, kwani Shirika linahitaji kuendelea na kupata faida kupitia makusanyo haya,” alisema Naibu Waziri Ngonyani.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, Profesa Norman Sigala, ameiomba Serikali kuliondoa Shirika hilo kwenye orodha ya mashirika yanayotaka kubinafsishwa.

Alisema Serikali ikitekeleza jambo hilo, italiwezesha Shirika hilo kujiendesha kibiashara, kuzalisha faida na kukabiliana na changamoto za ushindani kwenye soko.

Pamoja na hali hiyo, alisema Shirika hilo limekuwa wabunifu katika utoaji wa huduma zake kwa wananchi kwa kutumia teknolojia za kisasa zaidi badala ya kutumia mifumo ya kizamani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo, Luteni Kanali mstaafu Haruni Kondo, aliiomba kamati hiyo kuendelea kushirikiana na Shirika hilo na kulisaidia ili liweze kutoa huduma kwa wananchi kwa wakati na kwa ufanisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles