28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

SHIRIKA LA NDEGE ETIHAD LAPATA BOSI MPYA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


SHIRIKA la Anga la Etihad limetangaza uteuzi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Idara yake tanzu ya Airline Equity Partners, Robin Kamark, ambaye atashughulikia kuongoza na kuendeleza mikakati ya uwekezaji inayojumuisha wabia wa Shirika hilo.

Wabia hao ni Airberlin, Alitalia, Jet Airways, Air Serbia, Air Seychelles, Etihad Regional na Virgin Australia.

Mtendaji huyo mkuu atakuwa chini ya Rais wa Shirika hilo na Mkurugenzi Mkuu,  Kamark, anayechukua nafasi ya Bruno Matheu ambaye alishika wadhifa huo tangu Mei,  2016 na kuachia ngazi mwaka huu kwa sababu zake binafsi.

Kamark amefanya kazi katika sekta ya anga kwa takriban miaka 17, huku akifanikiwa kufikia malengo ya mikakati yake ya kibiashara na masuala ya utawala katika Shirika la SAS, ambako pia alikuwa akitekeleza majukumu yake kama Ofisa Mkuu wa Biashara.

Kwa miaka mitano yake ya mwishoni amefanya kazi kama Makamu wa Rais na Ofisa Mkuu wa Biashara katika kitengo cha bidhaa za ASA, zinazoongoza kwa huduma za kifedha na biashara.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Anga la Etihad, Mohamed Mubarak Fadhel Al Mazroue, alisema: “Shirika hili linaendelea kuwekeza duniani katika kiwango chenye ubora wa juu, ikiwamo kujenga timu nzuri itakayoongoza biashara na kuipelekea katika hatua kubwa zaidi za maendeleo.

“Robin ni kiongozi anayeheshimika katika sekta ya anga duniani, pia ana uzoefu mkubwa kutoka Shirika la SAS. Amefanya kazi kubwa ya kuboresha shirika hilo la ndege. Hivi karibuni amepanua wigo wa taaluma yake katika masuala ya huduma za kifedha.

“Ushirikiano na kampuni yetu utaendelea kuwa alama muhimu katika biashara na Robin ataongoza mipango hiyo kwa kuweka mikakati na kuendeleza dhamira yetu,” alisema.

 

Kutokana na hali hiyo, mwenyekiti huyo alimshuruku Bruno kwa juhudi zake kubwa alizoonyesha kwa kipindi cha miaka miwili na nusu kutokana na kufanikiwa kujenga na kuimarisha ushirikiano katika kitengo cha Airline Equity Partners.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles