24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Shirika la Candy kuwawezesha wanawake, makundi maalumu kiuchumi

Safina Sarwatt, Moshi

Zaidi ya Dola za Marekani milioni 10, zimetengwa na Shirika lisilo la kiserikali la Candy and Candy Group Limited, kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi vikundi vya wanawake wajane, watoto waishio katika mazingira magumu na vijana walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo jana mjini Moshi, Meneja wa shirika hilo, Fortunate Macha, amesema lengo la shirika hilo ni kuwasaidia makundi hayo kujikwamua kichumi na kuondokana na hali ya umaskini.

“Shirika limetenga fedha hizo kwa makundi hayo ili kuwasaidia kujikwamua kichumi na kuanzisha biashara mbalimbali itakayowawezesha kuwaongezea kipato.

“Mradi huo kwa mkoa Kilimanjaro unatarajia kuanza katika vijiji vya Kata ya Pasua na Kahe wilayani Moshi na kuendelea,” amesema.

Kwa upande wake Ofisa Mradi wa shirika hilo, Elizabeth Sabula, amesema mradi huo pia unatarajia kufikia vijana zaidia 200 wenye vipaji vya uimbaji.

Akizungumza kwa niaba ya Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kilimanjaro, Gerald Sakaya, aliipongeza shirika la hilo kwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia makundi hayo kuondokana na umaskini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles