29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Shime: Juhudi za wachezaji zimeleta mafanikio

Bakari Shime
Bakari Shime

NA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’, Bakari Shime, amesema juhudi zilizofanywa na wachezaji katika mchezo wa juzi dhidi ya Shelisheli ndiyo siri ya mafanikio ya ushindi walioupata.

Serengeti Boys juzi ilianza vyema kampeni zake kwenye michuano ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana (Afcon 17), baada ya kuichapa Shelisheli mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Shime aliliambia MTANZANIA jana kuwa wachezaji walicheza kwa kujituma na kuonyesha juhudi binafsi uwanjani jambo ambalo lilichangia kwa kiasi kikubwa kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani.

“Hakika wachezaji walizingatia mambo muhimu waliyokuwa wakifundishwa na kufuata maelekezo waliyopewa na benchi la ufundi hali iliyosaidia kurahisisha mbinu za kuwasoma wapinzani na kutumia mapungufu yao kuibuka na ushindi,” alisema.

Akizungumzia maandalizi ya mechi ya marudiano itakayochezwa Julai 2, mwaka huu ugenini, Shime alisema wachezaji wamepewa mapumziko ya siku mbili lakini kesho wataingia tena kambini kujiwinda na mchezo huo.

Katika mchezo wa marudiano, Serengeti Boys inahitaji matokeo ya ushindi au sare yoyote ili iweze kutinga raundi ya pili ya michuano hiyo ambapo itakutana na Afrika Kusini.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles