30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Shilole, Rostam kufanya kazi pamoja

 JESSCA NANGAWE 

BAADA ya msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kuachia ngoma yake ya ‘Pindua Meza’ sasa amekiri ni zamu ya kufanya kazi na rafiki zake wa karibu wanaounda kundi la Rostam ambao ni Roma na Stamina. 

Alisema licha ya ukaribu wake na kundi hilo walikuwa wanatumia muda mwingi kufanya mambo ya utani, lakini safari hii amekuja na wazo la kufanya nao kazi. 

Alisema tayari wamefanya mazungumzo na kukubaliana nao na wakati wowote mashabiki zao wapokee kazi hiyo. 

“Unajua wengi wanatuona tuna utani sana mimi na kina Roma lakini kuna wakati lazima tuonyeshe sisi ni watu wa aina gani linapokuja suala la kazi, nimekuja na wazo la kufanya ngoma ya pamoja na nimewapa masharti kabisa ya mimi kufanya kiitikio tu,”alisema Shilole. 

Ukaribu wa Rostam na Shilole umekua wa muda mrefu hali iliyowafanya kundui hilo wakati mwingine kumtumia Shilole katika baadhi ya mistari pale wanapotoa kazi yao mpya. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles