SHILOLE AENDELEZA URITHI WA MAMA YAKE

0
884

NA ESTHER GEORGE-DAR ES SALAAM


shiloleUNAJUA biashara ya kupika inalipa kiasi gani? Muulize Zuwena Mohammed (Shilole), kwani kitu hicho ndicho kilichomfanya msanii huyo achukue biashara hiyo aliyokuwa akiifanya mama yake.

Shilole aliliambia MTANZANIA kwamba, kama wasanii wasichana wangejua faida ya biashara ya chakula wangewekeza huko kwa kuwa inalipa licha ya kudharaulika na baadhi ya watu.

“Naipenda biashara hii kwa kuwa inalipa, lakini pia ni urithi kutoka kwa mama yangu hivyo naifanya kwa faida nyingi, inalipa na inanikumbusha enzi za mama alipokuwa akifanya biashara hii huku akinifundisha, sitaiacha na muziki nitaendelea nao,” alisema Shilole.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here