24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

SHIDA YA MATIBABU KWA WATANZANIA KUWA HISTORIA

Na MWANDISHI WETU


BINADAMU yeyote anahitaji kuishi maisha bora na yenye tija ikiwa ni pamoja na kuepuka majanga mbalimbali.

Ajali na maradhi ni kati ya majanga yanayowapata binadamu na wakati mwingine ikawa vigumu kuyazuia kutokana na asili yake. Lakini je, ni namna gani binadamu anatakiwa kujipanga kukabiliana na hali kama hiyo inapotokea?

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo inatajwa kuwa na sifa moja kubwa ambayo ni ubunifu. Sifa hiyo huenda  imeipa jina kubwa kibiashara na kujipatia watumiaji wengi wa mtandao huo, na huduma zake nyingine.

Miaka mitano iliyopita, kampuni hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Milvik Tanzania ilianzisha huduma ya bima ya afya inayoitwa BimaMkononi.

Haikuwa rahisi kwa Watanzania kujiunga na huduma hiyo, lakini kwa sasa kila mtumiaji wa Tigo anatamani kujiunga na huduma hiyo kutokana na uhalisia wake.

Hadi sasa wateja hai zaidi ya 200,000 wamejiunga na huduma hiyo, ambapo sharti kubwa la mteja ni kuwa mtumiaji wa huduma ya Tigopesa. Haihitaji kuwa na kitambulisho zaidi ya namba ya simu ambayo ndiyo inayomtambulisha mteja pale anapojisajili.

Mteja wa huduma hii atalazimika kupiga namba maalumu pale anapotaka kudai fidia baada ya kuumwa au kupata ajali, ili Tigo iweze kulipa katika hospitali au kituo chochote cha afya pale muhusika alipohudumiwa. 

Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu za Mkononi wa Tigo, Ruan Swanapoel  anasema BimaMkononi ni mfumo mpya wa bima unaowawezesha kuwakinga dhidi ya matukio yasiyotarajiwa, yanayoweza kuwa na athari kubwa kwa hali ya kifedha kama wasingekuwa wamejiunga na huduma au mpango huu wa bima. 

“Wakati tunaazisha huduma hii tulilenga kuwapunguzia tabu wanayoipata Watanzania wa kawaida pindi wanapopata matatizo kama ajali na kuugua. Kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa,” anasema Swanapoel.

Anafafanua kuwa ndani ya miaka mitano ya huduma hiyo kumekuwa na ufanisi mkubwa kutokana na jinsi ambavyo wateja wamekuwa wakilipwa fidia zao pale wanapopata matatizo.

“Mambo tunayoyafanya na ambayo  yanatuongezea sifa  katika huduma hii ni pamoja na uwepesi wa kuwalipa fidia wateja wetu pale wanapokuwa wamepata matatizo. Hili ndilo linawavuta wengine kama ndugu na marafiki wa wale wahusika kujiunga na huduma hii,” anafafanua Swanapoel.

Kwa mujibu wa meneja huyo, tayari BimaMkononi ishalipa fidia ya zaidi ya Sh milioni 27 katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Saidi Kamote, mkazi wa Lindi anasema yeye binafsi aliamua kujiunga na huduma hiyo baada ya kushuhudia ndugu yake alikipiwa fidia kwa gharama alizozitumia baada ya kuumwa na kulazwa hospitali kwa muda wa siku tatu.

Kamote anadai kuwa wakati ndugu yake anaugua familia yao ilikuwa katika wakati mgumu kifedha, lakini baadaye walirejeshewa fedha zao, baada ya kufuata taratibu zote za kudai fidia.

“Mwanzoni baada ya huyu ndugu yangu kutoka hospitalini, tulianza kushauriana jinsi ya kuanza upya tena kutafuta kipato, mimi ndio nilikuwa nae muda wote akiumwa, halafu ghafla akakumbuka hiyo BimaMkononi.

“Tuliwasiliana nao, wakatupatia maelekezo ya vithibitisho ambavyo tunatakiwa kupeleka, ikiwapo fomu maalumu za huko hospitali, baada ya hapo ilichukua kama siku tatu, akawa amefidiwa fedha tuliyotumia wakati anaumwa na maisha yakaendelea kama kawaida. Binafsi sasa hivi nimeshajiunga na huduma hiyo,” anaeleza Kamote.

Kwa upande wake Meneja wa Milvik Tanzania, Tom Chaplin anasema huduma ya BimaMkononi imetengenezwa makusudi  kutoa bidhaa za bima kwa Watanzania wote ambao  vinginevyo wasingeweza  kumudu huduma hiyo katika hali ya kawaida, pale wanapopata matatizo, ajali au kuugua.

“Huduma hii inafikia wateja kupitia simu za mkononi kusaidia  kufikiwa kwa urahisi  kadri inavyowezekana kwa wakazi wa  mjini na vijijini. Bima Mkononi  hadi sasa imekuwa na matokeo makubwa  katika kuogeza kazi ya mzunguko wa fedha ndani ya  sekta isiyo rasmi kwa kuwawezesha Watanzania  kuzifikia  huduma  za bima wanazozimudu  kutoka ndani ya simu zao.

“Lakini pia jambo jingine la fahari katika BimaMkononi, mteja hachaguliwi sehemu ya kupata huduma kwa maana ya hospitali. Kwa hili tumetoa uhuru kuwa kila mtu atibiwe anapotaka ila tupate taarifa kwa utaratibu tuliojiwekea ambapo kuna fomu maalumu zinatakiwa kujazwa baada ya mteja wetu kufidiwa au kulipiwa gharama alizotumia,” anasema Chaplin. 

Tom Chaplain  anaeleza kuwa  huduma hiyo imetengenezwa  mahsusi kwa  kuwapatia watu wote bima za maisha, hospitali na huduma binafsi ya ajali ambazo zinaweza kuzisaidia familia zao  kusimamia madhara ya kifedha ambayo yanaweza kusababishwa na matukio yasiyotarajiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles