26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

SHIBUDA: WANASIASA CHUNGENI NDIMI

KATIBU Mtendaji wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda

Na Mwandishi Wetu-Dodoma

KATIBU Mtendaji wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda, amewataka wanasiasa na viongozi wastaafu wa Serikali kuacha tabia ya  kujenga dhana inayokuza  mpasuko kwa jamii kwa kuwa makini na kauli zao.

Hayo aliyasema   mjini hapa jana kutokana na kauli ya Waziri Mkuu wa

zamani, Edward Lowassa   ya kuwatetea masheikh wa Jumuiya ya Mihadhara (Umasho) kuwekwa mahabusu kwa miaka kadhaa bila kesi yake kuamuliwa kuwa uonevu.

Shibuda alidai kauli ya Lowassa imekosa umakini na kutozifanya hoja zake zikose  uhalali .

“Wanasiasa ni vema wajenge fikra na kauli zenye umakini, hekima na mafunzo ya utetezi wa haki kwa kufuata  usawa bila ya kuongeza chumvi  au shinikizo la  mgawanyiko katika jamii.

“Masuala yanayobeba tuhuma za uhalifu au jinai ni vema vyombo husika vikapewa nafasi ili kujitosheleza na kujiridhisha katika taaluma,” alisema.

Shibuda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini,  alisema katika hoja iliyoibuliwa na Lowasa kuhusu waislamu,  mtu mwenye weledi na umakini itawia vigumu kubaini maono yake, shabaha na kusudio lenye msingi dhidi ya madai hayo kwa sababu  ni vigumu mtu mmoja kusafiria farasi wawili kwa wakati mmoja.

“Dira ya siasa ilenge katika kuleta mapinduzi ya fikra na uchumi kwa kuzingatia matumizi  salama ya matamshi, mipaka ya utawala iwe na rutuba ya kuhami rasilimali  jamii inufaike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles