30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Shibuda apigia chapuo uchaguzi Serikali za Mitaa

Mwandishi Wetu, Dodoma

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa nchini, John Shibuda, amewataka Watanzania wajitokeze kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika Jumapili Novemba 24, mwaka huu.

Pamoja na hali hiyo amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuchagua kiongozi anayemtaka kwani hatua hiyo itasaidia kujenga misingi ya utawala bora katika upatikaji wa viongozi hao.

Shibuda amesema hayo leo Ijumaa Novemba 22, leo kupitia taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari ambapo amewataka Watanzania kujitokeza na kwenda kupiga kura kuchagua viongozi hao pamoja na wajumbe wao.

“Natoa wito kwa umma wote mjitokeze na kwenda kupiga kura. Wito unazingatia kwamba kamati ya uongozi ya baraza la vyama vya siasa tayari imechukua hatua ya kusimamia kutendeka kwa hatua za kutakatisha hitilafu zote, zinazoathiri sifa za uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019.

“Kwa hiyo sasa, nashauri kila mtu mwenye sifa za kupiga kura na alikuwa amekwazika na kero za watendaji waitwao waborongaji wa kanuni za uchaguzi huu. Sasa nawashauri watu wote  muwe na ufikiri mwema wa kuunda uamuzi mpya wa kushiriki katika uchaguzi huu wa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa. Kwa hiyo jitokezeni mkapige kura siku ya Novemba 24,” amesema Shibuda.

Pamoja na mambo mengine, amewataka wananchi, wanasiasa na wakereketwa wa demokrasia na siasa za ushindani wa vyama vingi kutambua kwamba kususia upigaji kura si ubani wa sadaka ya kafara la kuondoa matendo batili ya kuundika kwa mazalia ya hila za athari za kiini macho kwa haki na usawa za mfumo wa vyama vingi.

“Ukombozi dhidi ya tabia za matendo ya watekelezaji maovu ya hulka potofu, dawa yake ni vikao vya kukosoana tupate masahihisho ya kujenga. Stahiki katika utungwaji wa kanuni mpya za uchaguzi.

“Kwa hiyo sasa, nawashauri wananchi, viongozi wa siasa na wakereketwa wa siasa kataeni kuwa mateka wa hasira za kuwapa ushindi waborongaji na waparaganishi wa kukwaza dhamiri zenu za kushiriki katika upigaji kura,” amesema.

Shibuda ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa vyama vya CCM na Chadema kwa nyakati tofauti, amesema Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa  ndiyo sauti kuu, hivyo vikao hivi vitawaarifu kuhusu matokeo ya kikao cha majadiliano na wasimamizi wa uchaguzi huu wa serikali za mitaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles