31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Sheria ya mimba kwa wanafunzi ifunzwe kwa wote

Said Meck Sadiki
Said Meck Sadiki

TANGU wiki iliyopita kumekuwapo na habari kuhusu uzembe katika kushughulikia wale wanaowapa mimba wanafunzi na kuwafanya wanafunzi hao wasiendelee na masomo.

Kwa mfano, iliripotiwa kuwa wanafunzi 238 wa shule za msingi na sekondari mkoani Kilimanjaro wamekatisha masomo baada ya kubainika kuwa ni wajauzito tangu Januari hadi Agosti, mwaka huu. Idadi hii ni kwa mkoa mmoja tu kwa muda wa miezi minane tu!

Serikali mkoani humo imeliagiza jeshi la polisi kuacha kufanyakazi kwa mazoea na kuhakikisha inawakamata watuhumiwa wote waliohusika kuwapa ujauzito wanafunzi hao, na kisha kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, alitoa kauli hiyo wakati wa sherehe za kuwapongeza na kuwakabidhi zawadi maofisa 34 wa jeshi la polisi waliohitimu kozi za uongozi hivi majuzi.

Tunasema huu ni mkoa mmoja wa nchi. Hali ya Tanzania kwa ujumla wake ni mbaya kuhusu suala hili.

Tunasema Serikali haina budi kulisimamia hili ili mimba za ovyo kwa wanafunzi lifike mwisho. Itoe mafunzo kwa watu wote waijue sheria inayohusu mimba kwa wanafunzi kuanzia kwa wanafunzi wenyewe, walimu wao, wananchi na watu wengine ambao kwa namna moja au nyingine wanakutana na wanafunzi katika shughuli mbaimbali.

Elimu kuhusu kitu chochote ni miongoni mwa huduma zenye umuhimu mkubwa na wa pekee kwa ustawi na maendeleo ya maisha ya mwanadamu.

Katika kutambua umuhimu wa hili, Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ilianzisha mipango mbalimbali katika kueneza elimu katika huduma za jamii.

Mfano mzuri hapa ni kwamba katika sekta ya elimu, ulianzishwa mpango wa elimu kwa wote uliofahamika kama UPE (Universal Primary Education) kwa lengo la kuhakikisha kuwa watu wanapata elimu, hususan elimu ya msingi.

Mpango huu ulitoa fursa kwa watoto wote wa Kitanzania kupata elimu ya msingi inayofanana bila kujali hali za kiuchumi za wazazi wao.

Suala hili la usawa katika elimu liliwezekana kwa sababu shule zote zilimilikiwa na Serikali, hivyo kutoa elimu kama huduma.

Tunapendekeza elimu hii itolewe kama huduma na bure tangu shule za msingi hadi chuo kikuu. Elimu hii ipewe kipaumbele na kwa kuwekewa umuhimu wa kutosha.

Katika kutambua umuhimu wa elimu, Mwalimu Nyerere, ilianzisha mipango mbalimbali katika maeneo nyeti katika  huduma za jamii.

Ni katika kipindi cha uongozi wake; maradhi, ujinga na umasikini vilitangazwa kuwa maadui wakubwa wa maendeleo ya Taifa letu. Na sisi kwa sasa tutangaze kuwa mimba mashuleni ni mojawapo wa maadui wa maendeleo yetu.

Tumesema mwanzoni kuwa kumekuwapo na habari kuhusu uzembe katika kushughulikia wale wanaowapa mimba wanafunzi na kuwafanya wanafunzi hao wasiendelee na masomo.

Lakini pia tunasema kuwa sheria kuhusu mimba kwa wanafunzi ielezwe au mafunzo yatolewe na kueleweka kwa kila mtu – wanafunzi wote, walimu, wananchi na wote ambao katika kufanya kazi zao hukutana na wanafunzi.

Tunasema hii itasaidia kila mtu kujua madhara yanayotokana na kupata mimba kwa mwanafunzi. Hali hii itachangia kuzuia mimba za ovyo shuleni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles