25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

SHERIA YA HABARI YAPINGWA MAHAKAMANI

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana baada ya kufungua kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) kupinga baadhi ya vifungu vya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari namba 12 ya mwaka 2016 vinavyokandamiza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza vifutwe. Kulia ni Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba na kutoka kushoto ni Wanasheria Jebra Kambole, Jenerali Ulimwengu na Mkurugenzi wa Watetezi wa Haki za Binadamu Onesmo Ole Ngurumwa.

Na CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

BARAZA la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria za Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), wamefungua kesi Mahakama ya Afrika Mashariki (EAC), kupinga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari namba 12 ya mwaka 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, kwa niaba ya viongozi wa taasisi hizo, alisema wameamua kufungua shauri kwa sababu sheria hiyo inanyima uhuru wa habari na kukandamiza demokrasia.

Mukajanga alisema shauri hilo namba 2 la mwaka 2017, tayari limesajiliwa na litafikishwa mbele ya mahakama iliyopo jijini Arusha.

Alisema sheria hiyo ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 5, mwaka jana na kuridhiwa na Rais Dk. John Magufuli.

Mukajanga alisema timu ya wanasheria Fulgence Masawe, Donald Deya, Jenerali Ulimwengu, Jebra Kambole, Francis Stola na Mpale Mpoki wanaziwakilisha taasisi hizo mahakamani.

“Washirika wanataka baadhi ya vifungu vya sheria hii ambavyo vinakandamiza uhuru wa habari wa kujieleza vifutwe, vinakiuka mkataba wa EAC ambao umeeleza nchi mwanachama kuzingatia na kulinda haki ambazo zimeelezwa katika mkataba huo Ibara ya 6 (d), na 7 (2),” alisema Mukajanga.

Alisema ibara ya 6 (d) ya Mkataba wa EAC, inahimiza umuhimu wa kufuata kanuni za utawala bora, utawala wa kidemokrasia, utawala wa sheria, uwajibikaji, uwazi, haki kwa wote, usawa wa kijinsia, pia kulinda na kuheshimu haki za binadamu.

Alisisitiza kuwa pia ibara ya 7 (2) ya mkataba huo, inaitaka nchi mwanachama kufuata na kuheshimu kanuni za utawala bora, ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni za kidemokrasia, utawala wa sheria na haki kwa wote.

Alisema kama ilivyo kwenye kifungu cha 8 (1), Tanzania inatakiwa kuchukua hatua za kuhakikisha haki zote zinazotajwa katika mkataba huo zinafuatwa na kutekelezwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles