25.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 31, 2023

Contact us: [email protected]

Sheria mpya yasomba NGO’S 250

ASHA BANI-DAR ES SALAAM

MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali 258 yamefutwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kutokana na kufanya majukumu kwa mujibu wa sheria ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs).

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rita, Emmy Hudson, alisema kufutwa kwa NGO hizo kwenye muunganisho wa wadhamini wa taasisi zenye kufanya shughuli zilizoainishwa kwenye sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali sura namba 56, ni kufuatia mabadiliko madogo ya sheria.

Alisema kuwa mabadiliko hayo yamefanyika katika sura ya 318 kupitia sheria ya marekebisho mbalimbali Na.3 ya mwaka 2019 iliyoanza kutekelezwa Juni 30 mwaka huu.

“Kuanzia sasa jukumu la kusajili muunganisho wa wadhamini utafanyika kwa taasisi zile tu ambazo zitakuwa katika utaratibu maalumu, ikiwa ni pamoja na taasisi ambazo usajili wake wa awali umefanyika kwa mujibu wa sheria nyingine, lakini zinahitajika kupata utu wa kisheria.

“Taasisi hizo ni pamoja na vyama vya siasa, mashirika na taasisi za kidini na vilabu vya michezo,’’ alisema.

Aliongeza kuwa taasisi ambazo usajili wake moja kwa moja hufanyika Rita ni zile zinazofahamika kama mifuko inayotoa huduma bila ya kupata faida na usajili wake unafanyika chini ya sheria ya muunganisho wa wadhamini sura ya 318.

Pia alisema taasisi ambazo usajili wake umetokana na maelekezo ya kisheria moja kwa moja au maamuzi ya kimahakama yanayoelekeza kuanzishwa kwa muunganisho wa wadhamini wa taasisi hiyo.

Emmy alisema taasisi zinazojihusisha na masuala ya kilimo ambazo hazijasajiliwa katika sheria yoyote ya Tanzania na zinahitaji usajili kwa ajili ya kupata utu wa kisheria.

 “Hivyo basi kuanzia siku ya tangazo hili, ofisi ya Mtendaji Mkuu  haitasajili tena muunganisho wa wadhamini wa taasisi yoyote ambayo inafanya  shughuli zilizoelekezwa kwa mujibu wa sheria ya NGO.

“Ijulikane kwamba kwa taasisi zile ambazo zilishasajiliwa Rita ambazo baada ya marekebisho ya sheria hizo zitafutwa rasmi katika daftari la muunganisho wa wadhamini katika ofisi ya Rita, wadhamini watapaswa kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha wanalipia madeni yote wanayodaiwa katika marejesho ya wadhamini kila mwaka kwa kipindi ambacho hawakulipa madeni yao walipokuwa Rita,’’ alisema.

Pia alisema wanatakiwa kurejesha hati halisi ya usajili wa wadhamini ambayo walikabidhiwa wakati wa usajili.

Baadhi ya mashirika hayo ni Muungano wa Wafugaji na Wawindaji nchini, Maarifa Media Trust (Mamet), Saint Anne Maria, Comprehensive Community Based  Rehabiliation in Tanzania (CCBRT), Mviwata Trust Fund na Human Right Resources Center of Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,315FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles