25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

SHERIA HUDUMA YA VYOMBO VYA HABARI YANG’ATA

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

SHERIA ya huduma ya habari inaonekana kuwa kitanzi kwa wanahabari na ustawi wa vyombo vya habari kwa ujumla wake, kutokana na kutokuwa rafiki katika baadhi ya maeneo.

Vyombo vya habari vinafahamika wazi kutegemea zaidi matangazo hasa kutoka serikalini na taasisi zake ili kuviendesha, lakini sheria hii inaonekana kudhibiti jambo hilo.

Katika sehemu ya Nne sheria hiyo inazungumzia uratibu wa matangazo ya Serikali, ikimpa mamlaka makubwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) kusimamia matangazo yote ya Serikali.

Matangazo hayo ni kutoka wizara, idara, wakala na taasisi za serikali pamoja na miradi, ambayo inachangia asilimia 50 ya fedha bila kusahau serikali za mitaa ambazo zinahusisha halmashauri mbalimbali nchini.

Kwamba Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo atahakikisha matangazo yote yanapitia kwake, akiwa na mamlaka ya kuruhusu au kuzuia pamoja na kuchagua chombo gani cha habari matangazo hayo yanapaswa kwenda.

Kifungu hicho kinamaanisha baadhi ya vyombo vya habari hasa vya binafsi na vile vinavyoonekana kuwa na mwelekeo wa kuikosoa Serikali vitarajie kukosa matangazo hayo.

Si hilo, kitendo cha Mkurugenzi kutwikwa zigo kubwa la kuratibu matangazo yote hayo, ni wazi kuwa kutakuwa na urasimu na ucheleweshaji mkubwa wa matangazo kutoka taasisi hizo.

Mbali ya hayo, ada anazotozwa mwanahabari hazionekani kuwa rafiki; kwa mfano mwandishi atatakiwa kulipia ada ya Sh 100,000 ili kupata kitambulisho kinachomruhusu kufanya kazi kwa muda wa miaka miwili ilihali hati ya kusafiria hudumu kwa miaka 10 kwa sh 50,000 tu.

Jingine wakati ikiwa imeweka kiwango cha diploma kuwa cha chini ili kuwa mwanahabari, wale wenye shahada zisizohusiana na uandishi wa habari watatakiwa kwenda kusomea diploma ya habari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles