24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

‘SHERIA HAIWATAJI WABUNGE VITI MAALUMU KUHUDHURIA KAMATI ZA FEDHA’

Ramadhan Hassan, Dodoma

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imesema sababu za wabunge wa Viti Maalumu kutoingia kwenye kamati za fedha katika halmashauri  ni kutokana na wabunge hao kutokutajwa katika sheria.

Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Taska Mbogo (CCM), aliyetaka kujua ni kwa nini wabunge wa viti maalumu hawaingii kwenye vikao vya kamati za fedha za halmashauri zao.

Alisema wabunge wa Viti Maalum ni sawa na Wabunge wengine wa majimbo na hakuna tofauti ya kiapo cha wabunge wa majimbo na wale wa viti maalumU.

Akijibu swali hilo, Kakunda amesema kamati ya fedha, uongozi na mipango imeundwa kwa mujibu wa Sheria ya serikali za Mitaa(Mamlaka za wilaya) sura 287, kifungu cha 75 na Sheria ya serikali za mitaa(Mamlaka za miji), Sura ya 288 kifungu cha 47 pamoja na kifungu cha 40(2)(c) cha Kanuni za kudumu za Halmashauri za mwaka 2014.

“Kanuni za kudumu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kifungu 41(1) zinataja wajumbe wa kuingia kwenye kamati hiyo kuwa ni Mea au Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye atakuwa Mwenyekiti, Naibu Meya au Makamu Mwenyekiti, Mbunge au wabunge wa majimbo,” amesema.

Naibu Waziri huyo alisema kwa sasa utaratibu utaendelea hivyo ikiwemo kutokutoa fedha za mfuko wa Jimbo kwa wabunge wa viti maalumu hadi hapo sheria itakapobadilishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,853FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles