25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

SHEPU FEKI ZATIKISA MASTAA BONGO

Na JOSEPH SHALUWA

MSANII ni mbunifu, anayefikisha ujumbe kwa hadhira kupitia sanaa (kipaji) aliyonayo/alichonacho. Inakusudiwa msanii afundishe, aburudishe na aonye jamii kupitia kazi yake.

Wapo wasanii wa aina nyingi. Msanii anaweza kuwa msusi, mchongaji, mchoraji, mtungaji, mwigizaji, msimuliaji, mshonaji, mchomeaji nk.

Kinachomtambulisha msanii kwenye jamii ni sanaa aliyonayo, basi! Ni ule utofauti alionao na wengine, maana msanii huwa na talanta au kipaji cha tofauti na wengine. Ule utofauti wake ndiyo usanii.

Lakini hali imekuwa tofauti kwenye jamii ya sasa, ambapo wasanii wa kweli wamepewa kisogo na kuachiwa wale wasio na vipaji kushika hatamu.

Hao ndiyo wanaofanya mambo ya ajabu kwa mwavuli wa sanaa kwa dhamira binafsi, tofauti na sanaa waliyojifichia. Lakini wapo wengine ni wasanii wa kweli ila kwa tamaa na kutaka mambo makubwa hujiingiza kwenye mambo yasiyo na maana kwenye usanii wao.

Stori iliyo gumzo kwa sasa miongoni mwa mastaa wa Bongo ni madai ya wasanii wa kike nchini kutumia makalio feki ili kuongeza mwonekano wao kwa lengo la kuvutia na kuonekana warembo zaidi.

Madai ya mastaa kutumia makalio bandia huku wengine wakidaiwa kutumia dawa za kukuza makalio yapo muda mrefu nchini na hata nchi za wenzetu, lakini mastaa wengi wamekuwa wakikanusha madai hayo.

 

SHEPU FEKI

Inadaiwa kwamba, wapo warembo mastaa (na hata wasio mastaa) ambao kwa kupenda kuwa na mionekano mizuri huamua kutumia vifaa maalumu vya kuwafanya waonekane wana shepu nzuri zaidi ya walizojaliwa.

Madai yanasema kuwa, zipo taiti zenye sponchi, ambazo huongeza mwonekano wa sehemu za makalio na hips ambazo mwanamke akivaa, humbadilisha mwonekano wake.

Mbali na matumizi ya taiti hizo, madai mengine yanaeleza kuwa zipo dawa za Kichina ambazo huongeza makalio, hips na sehemu za matiti na hivyo baadhi ya mastaa huzichangamkia ili kuongeza urembo na mionekano mbele ya mashabiki.

 

WEMA, LULU WATAJWA

Mastaa wengi wanadaiwa kuwa kwenye mkumbo wa kubadilisha mionekano yao. Mastaa bei mbaya Bongo, Wema Sepetu na Elizabeth Michael ‘Lulu’ wanaotesa kwenye filamu, wamekuwa gumzo kwa siku kadhaa sasa wakijadiliwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii wakihusishwa na madai hayo.

Mbali na mitandao ya kijamii, jarida moja la burudani mwishoni mwa wiki iliyopita liliripoti madai hayo ambayo yalihusisha minong’ono ya kwenye mitandao ya kijamii baada ya shepu za mastaa hao kushtua.

Mjadala mkubwa uliibuka baada ya Wema kuposti picha zake mpya zinazomwonyesha akiwa kwenye mwonekano uliozua mjadala mkubwa.

Wapo waliohoji kuhusu mwonekano wake huo, huku wengine wakimtetea kwamba shepu yake ndivyo ilivyo na hajatumia taiti za kuongeza makalio wala dawa za Kichina.

Wema mwenyewe akionekana kuwajibu wanaomdisi kuhusiana na shepu yake hiyo, alisema: “Nawashangaa sana wanaojadili umbo langu kila kukicha, hawajui mimi nina umbo siyo la kawaida na kwetu tupo hivyo.

“Wamwangalie mama yangu watapata jibu lakini watu walivyo siyo waelewa utasikia nimetengeneza shepu, kwa sababu zipi nifanye hivyo?

“Niseme tu kwamba nimechoka kuambiwa hili kalio ni feki, I swear hili ni original na namshukuru Mungu kwa kuniumba hivi kwani kila nguo ninayovaa napendeza, navutia.”

Kwa upande wa Lulu, minong’ono ilianza baada ya kuonekana kwenye pati moja hivi karibuni akionekana hana mwonekano wake ule wa siku zote.

Hata hivyo Lulu hawajafafanua wala kujibu tuhuma hizo ambazo mpaka sasa hazina ushahidi wowote, zinabaki kama madai ya mitandaoni tu.

 

KIM KARDASHIAN

Minong’ono ya matumizi ya taiti za kuongeza mvuto au dawa za kuongeza ukubwa wa makalio zimewakumba pia mastaa mbalimbali duniani.

Mwanamitindo mwenye mvuto nchini Marekani, Kim Kardashian ambaye ni mke wa mwanamuziki Kanye West naye aliwahi kukumbwa na kashfa hiyo ambayo ilimtesa sana.

Katika kuwaonyesha mashabiki wake kuwa hana anachoongeza kwenye umbile lake, Kim aliamua kupiga picha za utupu na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii ili kuzima minong’ono ya madai hayo.

Baadaye Kim alipiga picha nyingine na kutoka katika jarida moja la nchini Uingereza.

 

MASTAA SOMENI HAPA

Swaggaz linawapongeza mastaa wote wa kike nchini wenye juhudi na ubunifu katika sanaa. Miongoni mwa mastaa wa kike ambao Swaggaz linawakubali kutokana na kazi zao zilizotukuka ni Wema na Lulu.

Tunawasihi watulie na wasifikirie kufanya kama Kim ili kudhihirisha kuwa hawapo kwenye mkumbo wa matumizi ya ‘madude’ hayo ya kuongeza mvuto. Lakini pia wasifikirie kabisa kutumia dawa wala taiti hizo.

Mastaa wote wa Bongo – waliohusishwa na madai hayo na wale ambao hawajatajwa, ni vizuri kujiamini na kukubali uwezo wao kisanii kuliko kufikiria mwonekano wa nje.

Kwa kawaida siyo rahisi kubadili mwonekano uliojaliwa na Mungu, zaidi utajiharibu badala ya kujitengeneza. Ridhika na ulivyo, kisha ongeza bidii kwenye sanaa, utazidi kung’aa na kuwa staa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles