23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

SHEIKHATANGAZA KUMSHTAKI MANGE KIMAMBI KWA MUNGU

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Salum, amesema atafanya dua maalumu kumshitaki kwa Mungu, mwanadada maarufu mitandaoni ambaye anaishi Marekani, Mange Kimambi, kwa kumtukana katika mitandao ya  jamii.

Amesema pia kuwa ataufikisha katika vyombo vya sheria mtandao wa Jamii Forums kwa kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa na mhusika.

Kauli hiyo ya Salum imetolewa siku chache baada ya Mange kuweka picha katika ukurasa wake wa Instagram, ikimuonyesha Sheikh Salum akiwa   na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwamo mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia.

Mange alimshutumu Sheikh Salum kwa kumfanyia kampeni mgombea huyo wa CCM Kinondoni wakati sheikh huyo aliwahi kuwaasa viongozi wa dini wasijihusishe na siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Sheikh Salum alisema mwaka huu utakuwa wa mwisho kwa mwanadada huyo kutukana watu na hatabaki salama.

“Tutarejea katika mahakama ya mbinguni na kumwuliza Mungu kama viungo alivyompa Mange vilikuwa kwa ajili ya kutukana watu na kuwadhalilisha tu,” alisema Sheikh Salum.

Alisema taarifa hizo ambazo hazina ukweli pia zimetumwa katika mtandao wa Jamii Forums, bila kuthibitishwa hivyo wataufikisha mtandao huokatika vyombo vya sheria.

“Jamii Forums wamepost pia taarifa hizi na picha zangu kuwa ninapiga kampeni hii… si kweli hivyo tutawashtaki katika vyombo vya dola,” alisema Sheikh Salum.

Kiongozi huyo wa dini alisema hiyo ni mara yake ya kwanza na ya mwisho kujibizana na mwanadada huyo na hatasikia tena akimjibu.

“Tulikuwa katika msiba wa Sheikh Masoud Ismail pale Kijitonyama ndipo walipokuja Mtulia na wafuasi wake wakawa wanapiga picha na mimi wala sijawahi kufanya kampeni,” alisema Salum.

Akizungumza kwa masikitiko, alisema Mange amekuwa akiwadhalilisha viongozi wakubwa na sasa hawatavumilia kuona anawatukana na viongozi wa dini.

“Hapa amegusa pengine na acheze kwingine si katika mahakama ya mbinguni, huu ni mwaka wake wa mwisho kutukana,” alisema Sheikh Salum.

Aliwataka watanzania kuacha kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa na wahusika kwa sababu  kufanya hivyo ni kujipalia moto.

Baada ya kauli hiyo ya Sheikh Salum, Mange naye alimjibu katika ukurasa wake wa Istagram, akiandika: “Mwenyezi Mungu akipokea dua yako wewe ili mimi nidhurike, basi hata dua zangu  zitapokelewa.”

Wakati huo huo, Sheikh Salum alilipongeza Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam kwa kupata kiongozi mpya.

“Mimi kama mwenyekiti wa kamati ya amani ya mkoa nina imani kuwa tutashirikiana naye katika kuhakikisha mkoa huu unakuwa na amani,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles