21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

SHEIKH DAR AMKINGIA KIFUA MAGUFULI

maguuli2Na LEONARD MANG’OHA – DAR ES SALAAM

SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, amevishutumu baadhi ya vyombo vya habari vinavyoandika habari alizodai kuwa zina nia ya kumgombanisha Rais John Magufuli na viongozi wa dini.

Shutuma hizo alizitoa jana katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake Dar es Salaam, aliouitisha mahususi kuzungumzia hatua iliyofikiwa na viongozi wa dini waliotia nia ya kukutana na Rais Magufuli kuzungumzia mwenendo wa kisiasa nchini.

Alisema taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais Magufuli amekataa kukutana na viongozi wa dini si za kweli na kwamba uamuzi huo haukutokana na maombi ya viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Sheikh Salum alisema ni kweli viongozi wa dini walikutana na viongozi wa Ukawa  wakawaomba wasitishe azma yao ya kufanya maandamano na mikutano nchi nzima ikiwa ni utekelezaji wa operesheni iliyopachikwa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta (Ukuta).

Alisema katika mkutano huo, viongozi wa dini waliwaomba Ukawa wawaruhusu wabunge kurejea kushiriki vikao vya Bunge la Jamhuri jambo ambalo waliliridhia na kwamba baada ya makubaliano hayo, viongozi hao wa dini kwa utashi wao waliazimia kukutana na Rais Magufuli.

“Baada ya kikao hicho jukumu la kumtafuta Rais kuzungumza naye lilibaki mikononi mwetu jambo ambalo hadi sasa halijafanyika lakini tunashangaa kuona baadhi ya vyombo vya habari vinatoa taarifa za uongo kabla hata hatujamwandikia barua Rais ya kukutana naye.

“Huku ni kumgombanisha Rais na viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla. Ukweli ni kwamba barua imeandikwa na viongozi wa dini kwa mheshimiwa Rais tarehe 19/09/2016 na kupelekwa siku hiyo hiyo.

“Rais anawaheshimu viongozi wa dini na amekuwa akiwaomba wamwombee na anawapenda sana hivyo hawezi kuombwa kuonana na viongozi hao akatae,” alisema Sheikh Salum.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles