25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

SHEHENA YA SAMAKI YAKAMATWA IKISAFIRISHWA SUDAN, SOMALIA

desktop-1451498746

Na SHOMARI BINDA-MUSOMA

SAMAKI wachanga 240,000 wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 9.3, waliokuwa katika harakati za kusafirishwa kwenda nchi za Sudan na Somalia, wamekamatwa katika Kijiji cha Bugunda wilayani Musoma.

Taarifa ya kukamatwa samaki hao, imetolewa juzi na Ofisa Mfawidhi Mdhibiti wa Rasilimali za Ziwa Victoria Mkoa wa Mara, Juma Makongoro, ambaye alisema iwapo samaki hao wangeachwa miezi mitatu ziwani wakakua wangeweza kuliingizia Taifa zaidi ya Sh bilioni tatu.

Alisema mhusika wa samaki hao baada ya kupata taarifa juu ya ujio wa maofisa uvuvi na askari nyumbani kwake alikimbia na familia yake na kuteketeza mji wake kwa moto, lakini vyombo vya ulinzi vinaendelea kumsaka.

Alisema taarifa ya mtuhumiwa kukausha samaki hao kwa ajili ya kuwasafirisha, walizipata kutoka kwa wasamaria wema.
Alisema samaki hao ni hasara kubwa kwa Taifa kwa kuwa walikuwa wachanga, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Kwa kweli samaki hawa wachanga ni wengi, wamevuliwa bila kuzingatia taratibu za uvuvi, hii inasababisha kupungua kwa kasi kubwa ya samaki Ziwa Victoria.

“Tunaendelea na operesheni ya kupambana na wavuvi wanaovua bila kuzingatia taratibu, tunashukuru wananchi ambao wamekuwa wakitoa taarifa zilizokuwa zikifanikisha kukamata wahalifu,” alisema Makongoro.

Akizungumza baada ya kupewa taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk. Charles Mlingwa, ameagiza kusakwa kwa mhusika huyo mchana na usiku na atakapopatikana afikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Alisema Serikali haiwezi kukubali kuona watu wachache wakifanya vitendo haramu kwa manufaa yao na kuhatarisha rasilimali zilizopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles