24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Shehena ya mizigo bandarini yaongezeka

  Na NORA DAMIAN -DAR ES SALAAM

SHEHENA mchanganyiko katika Bandari ya Dar es Salaam zimeongezeka na kufikia tani milioni 3.2 ikilinganishwa na tani milioni 2.9 katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Bandari hiyo ina uwezo wa kuhudumia shehena tanimilioni 13.5, lakini mwaka 2017/2018 ilihudumia tani milioni 16.4 hatua iliyosababisha kufanya upanuzi kwa lengo la kuiongezea uwezo wa kuhudumia mzigomkubwa zaidi.

Akizungumza juzi, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Fred Liundi, alisema mafanikio hayo yanatokana na maboresho yanayoendelea ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ufanisi.

Kwa upande wa makontena, alisema walihudumia 184,200 juu ya lengo la makontena 154,171 ikiwa ni ongezeko la makontena 26,971. Kiasi kilichohudumiwa mwaka uliopita katika kipindi kama hicho ni makontena 169,974.

“Yako masoko yanayohudumiwa na Bandari ya Dar es Salaam kama Zambia, DRC, Burundi, Rwanda na Uganda na tumehudumia asilimia 81.2 ya mizigo inayopitia bahari kuu kwenda katika nchi hizo,” alisema.

Kuhusu mapato, alisema katika kipindi hicho wamekusanya Sh bilioni 206.5 tofauti na Sh bilioni 202.2 walizopanga kukusanya.

Akizungumzia upanuzi unaoendelea katika bandari hiyo, alisema unahusisha kuongeza kina katika magati yaliyopo kwani yana kina kinachoanzia mita 8.5 hadi 10.5 ambacho ni kidogo kwa sababu teknolojia ya meliimebadilika na zinazotengenezwa sasa zinahitaji kina kirefu.

Alifafanua kuwa kina cha mlango wa bahari wa kuingilia meli kitaongezwa kutoka mita 10 hadi 15.5.

“Kulikuwa na haja ya bandari kuongeza uwezo wakuhudumia mzigo mkubwa zaidi, na kutokana na maboresho yanayoendelea tumeongeza muda wa kuhudumia meli kutoka siku tatu hadi 2.1 kwa upande wa kontena na siku2.8 kwa meli za mizigo isiyokuwa kwenye kontena,” alisema.

Hata hivyo alisema wana kabiliwa na changamoto yauwepo wa bandari bubu ambazo zina hatarisha usalama wa afya za wananchi nakuikosesha mapato Serikali.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, katika eneo la Dares Salaam, Pwani na Mafia tayari wamezitambua bandari bubu 71 na kati ya hizoWilaya ya Kigamboni ndiyo inaongoza kwa kuwa na bandari bubu 24, Temeke saba na Kinondoni nne.

 “Kutumia bandari zisizo rasmi ni kosa la uhujumu uchumi ndiyo maana tunafanya kila jitihada kuhakikisha tatizo lina dhibitiwa ili kupata kodi ya Serikali nakuimarisha usalama wa nchi kwa ujumla,” alisema Liundi.

Kuhusu meli za mafuta kuhudumiwa kwa muda mrefu,alisema wamepanga kuwa na kituo kimoja cha upakuaji wa mafuta kutoka kwenye meli kisha kusambazwa kwa mwagizaji mmoja mmoja.

Hivi sasa meli ya mafuta katika bandari hiyo inahudumiwa kwa siku 6.5 na malengo ya bandari ni kuhudumia kwa siku tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles