23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 10, 2022

Sharapova arudi rasmi kwenye tenisi

sharapovaLAS VEGAS, MAREKANI

BAADA ya kufungiwa katika mchezo wa tenisi kwa miaka miwili, Maria Sharapova ameonekana kwa mara ya kwanza juzi akicheza katika kuchangia mfuko wa Elton John AIDS.

Nyota huo raia wa nchini Urusi, alifungiwa kutoshiriki mchezo wa tenisi kwa miaka miwili kwa tuhuma za kutumia dawa za kulevya.

Hata hivyo, mwanamichezo huyo alikiri kuwa alikuwa anatumia dawa hizo kabla ya kukatazwa michezoni na alikuwa anatumia kutokana na matatizo yake ya afya.

Kutokana na tuhumu hizo, Chama cha Tenisi cha Kimataifa (ITF), kilikaa na kuamua kumpunguzia adhabu hiyo ambapo sasa anatakiwa kurudi rasmi kwenye michuano mbalimbali ifikapo Aprili mwakani.

Lakini juzi alionekana akicheza katika mchezo wa kuchangia mfuko wa Elton John AIDS na alionekana kuwa ni mtu wa furaha huku akiamini kuwa bado atarudi kwenye ushindani.

Sharapova akiwa na mchezaji mwenzake kutoka nchini Marekani, Taylor Johnson, walishindana na wapinzani wake, Martina Navratilova pamoja na Liezel Huber.

“Ilikuwa ni siku muhimu sana kwangu na mchezaji mwenzangu Johnson, kwa upande wangu nilikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, lakini baada ya kushuka uwanjani kwa mara ya kwanza ninashukuru kuwaona mashabiki wangu wakijitokeza kwa wingi.

“Nimefurahi sana kuona narudi kwenye mchezo huu kwa kuwa hii ni sehemu ya maisha yangu, nimefanya makubwa na natarajia kufanya makubwa zaidi nikirudi uwanjani,” alisema Sharapova.

Kwa mara ya mwisho kwa Sharapova kucheza tenisi katika ushindani ni katika michuano ya Australian Open, amedai kuwa bado anasumbuliwa na bega, lakini hadi kufika Januari mwakani atakuwa katika hali nzuri na atarudi katika tenisi kwa kishindo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles