22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

SHARAPOVA AMCHANA ‘LIVE’ MURRAY

LOS ANGELES, Marekani

MWANADADA Maria Sharapova, amemjia juu staa mwenzake katika mchezo wa tenisi, Andy Murray, akimwambia afunge mdomo kwani haelewi chochote kuhusu tuhuma zake za utumizi wa dawa za kuongeza nguvu.

Sharapova, mwenye umri wa miaka 30, aligundulika kutumia dawa hizo mwaka jana na ametumikia kifungo chake cha miezi 15 kabla ya kurejea mzigoni Aprili mwaka huu.

Hata hivyo, alijitetea kuwa amekuwa akitumia dawa hizo kwa zaidi ya miaka 10 kwa nia ya kutuliza maumivu na si kuongeza nguvu.

Tangu kurejea kwake, Sharapova amekuwa akikosolewa vikali na wanaomtaja kuwa si mfano wa kuigwa, akiwamo Murray.

“Sifikiri ni maoni yao kwa sababu hawajui lolote,” alisema Sharapova alipokuwa akihojiwa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC).

“Lakini mwisho wa siku, hii ndiyo kazi yangu, nilikabiliana na tatizo hilo, nilikubali kosa na kutumikia adhabu na sasa nimerudi.”

Mbali na Murray, pia mkali Eugenie Bouchard wa Canada, alimtaja Sharapova kuwa ni muhuni na alistahili kufungiwa kutocheza tenisi kwa kipindi chote cha maisha yake.

“Sidhani kama anayedanganya anatakiwa kuendelea kuwamo kwenye mchezo wowote. Ni kutowatendeea haki wale walio wasafi,” alisema Bouchard akimzungumzia Sharapova.

‘Nafikiri WTA (Chama cha Tenisi) hakijatuma ujumbe mzuri kwa chipukizi kwa kumkaribisha (Sharapova).”

Michuano ya kwanza kwa Sharapova tangu atoke kifungoni ni ile ya mwaka huu ya US Open ikiwa ni baada ya kuikosa Roland Garros na Wimbledon.

Katika mashindano hayo ya US Open, aliishia raundi ya nne baada ya kuchakazwa ma Anastasija Sevastova. “Ningependa kushinda mataji mengi zaidi na hilo ndilo lengo langu, kuna mambo mengi ningependa kuyakamilisha.

“Nafikiri wale wanaonikosoa hawana hoja, hivyo sina mpango nao,” alisema Sharapova ambaye hajashinda taji lolote la michuano mikubwa tangu alipobeba French Open mwaka 2014.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles