Sharapova afungiwa miaka miwili

0
868
Maria Sharapova
Maria Sharapova
Maria Sharapova

MOSCOW, URUSI

NYOTA wa mchezo wa tenisi, Maria Sharapova, amesimamishwa kushiriki katika mchezo huo kwa miaka miwili kutokana na kugundulika kwamba alitumia dawa zisizokubaliwa michezoni ambazo zinajulikana kwa jina la Meldonium.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, aliandika katika ukurasa wake wa facebook kwamba atakata rufaa kwa kile alichokiita uamuzi mkali aliochukuliwa na hakutendewa haki kutoka katika shirikisho la kimataifa la mchezo wa tenisi.

Sharapova alijitetea kuhusiana na matumizi ya dawa hizo aina ya Meldonium na kudai kwamba alifanya hivyo kwa sababu za kitabibu na ndio maana alitumia dawa hizo.

“Ni jambo la kuhuzunisha kufungiwa kwenye tenisi, ninaamini jina langu kuwa kubwa linatokana na mimi kufanya vizuri katika mchezo huu, lakini sikati tamaa nitarudi tena kwenye mchezo huu muda mfupi ujao kwa kuwa lazima nikate rufaa,” aliandika Sharapova.

Kabla ya kufungiwa kwa mwanamichezo huyo, kikosi cha timu ya Taifa ya Urusi ambacho kitaenda kwenye michuano ya kufukuza upepo ya Rio Olympic mwezi Agosti, jina la nyota huyo lilitajwa.

Kufungiwa huko kwa Sharapova kumeanza kuhesabiwa tangu Januari 26 mwaka huu hadi pale itakapokamilika miaka miwili, lakini inadaiwa kwamba anaweza kukata rufaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here