23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

SHANIA AWAOMBA MSAMAHA WAMAREKANI

CALIFONIA, MAREKANI


MWANAMUZIKI wa Marekani, Shania Twain, amelazimika kuwaomba msamaha raia wa nchi hiyo ambao walikerwa na maoni yake kuwa angependa kumpigia kura rais wa nchi hiyo, Donald Tramp, katika uchaguzi ujao unaotarajia kufanyika Novemba mwaka 2020.

Twain alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika mahojiano na gazeti la The Guardian la nchini Marekani.

Lakini baada ya kuandamwa na maoni ya raia wa nchi hiyo yaliyoonesha kuchukizwa na kitendo hicho, jana Twain aliomba msamaha katika kituo cha runinga cha E News.

“Napenda kumwomba msamaha kila mtu aliyechukizwa na maoni yangu niliyotoa katika mahojiano na gazeti la Guardian, maswali niliyoulizwa yalinitoa kwenye mstari.Mimi ni raia wa Canada, najuta kujibu swali hili bila kuzingatia uhalisia.

“Nilikuwa najaribu kuelezea kuhusu swali ambalo lilikuwa likihoji juu ya uchaguzi ujao, sikuwa na maana ambayo inatafsiriwa na watu wengi sasa, sikuwa na lengo la kumuumiza mtu yeyote, sina imani yoyote ya kawaida ya maadili na Rais wa sasa,” alisema Twain.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles