31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

SHANGWE ZA FIESTA KUHAMIA MUSOMA

Na MWANDISHI WETU

MSIMU mpya wa tamasha kubwa la burudani la Tigo Fiesta ulianzia mwishoni mwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, ambapo msanii Ali Kiba alifunika kutokana na wimbo wake wa Seduce Me, uliojizolea umaarufu.

Baada ya tamasha hilo kupagawisha wapenzi wa burudani wa Arusha, leo uhondo wa tukio hilo kubwa kabisa la burudani unahamia mjini Musoma, katika Uwanja wa Karume.

Wasanii wakali wa muziki nchini wanatarajiwa kukinukisha katika tamasha hilo la aina yake, ambalo mwaka huu limedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania.

Kwa mujibu wa waandaaji, Clouds Media, wasanii watakaopanda jukwaani kutoa burudani leo ni pamoja na Roma Mkatoliki, Rostam, Darassa, Stamina, Shilole, Nandy, Ben Pol, Jux na Saida Karoli.

Wasanii wengine ni Joh Makini, Fid Q, Stamina, Mr Blue, Ditto, Dulla Makabila na wengineo.

Kauli mbiu ya Tigo Fiesta mwaka huu ni ‘Tumekusoma’ na kwamba baada ya wasanii hao kuuwasha moto Musoma, Jumapili watahamia Kahama na burudani hiyo kuendelea katika mikoa ya Mwanza, Tabora na Dodoma.

Maeneo mengine ni Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Mtwara na kuhitimishwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kuhusiana na tamasha la mwaka huu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Fiesta, Sebastian Maganga, anasema kuwa, Tigo Fiesta ni burudani ya kipekee ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki na kwamba mashabiki wamefurahia burudani Arusha na wataendelea kufurahia zaidi katika mikoa mingine.

“Tutawaletea wasanii wenye hadhi kulingana na mapendekezo ya mashabiki husika wa mkoa huo, tena wale waliojizolea sifa ndani na nje ya nchi,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles