SHAMSA FORD: SURA ZA WANAUME HAZINISUMBUI

0
840

Na ESTHER GEORGE


MREMBO anayefanya vyema kwenye filamu nchini, Shamsa Ford, ameibuka na kuwataka wasichana wenye majina kuacha kuchagua wanaume wa kuwaoa kwa sura zao bali waangalie tabia zao.

Shamsa alisema wasichana wengi wamekuwa na tabia ya kupenda wanaume kwa sura zao, lakini yeye anashauri waangalie tabia zao.

“Natoa ushauri huu kwa wanawake wezangu hasa hao wanaojiona mastaa, mimi walinicheka kwa kumpenda Chidi Mapenzi lakini sijaangalia sura yake nimeangalia tabia na anavyoweza kumudu majukumu yake kama baba wa familia.

“Mwanamume bora ni yule mwenye malengo, umakini, misimamo na mwenye busara na si sura nzuri na hutimiza majukumu yake kama baba wa familia, pia wanawake tunatakiwa tuwe makini kuchagua mwananume sahihi,” alieleza Shamsa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here