Shamsa Ford akubali ombi la Chidi Mapenzi

0
2926

Na BEATRICE KAIZA

MSANII wa filamu nchini, Shamsa Ford, amemsamehe  aliyekuwa mume wake, Chidi Mapenzi baada ya mfanyabiashara huyo kutumia siku ya Wanawake Duniani kumwomba radhi kwa yote mabaya aliyomfanyia wakiwa pamoja.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Shamsa alisema amepokea ombi hilo na hana tatizo tena na mumewe huyo wa zamani kwakuwa  sasa kila mmoja anaishi maisha yake.

 “Sina tatizo na Chidi Mapenzi na nimemsamehe, sisi ni binadamu. Mungu amfungulie baraka na aendelee kuishi maisha yake vizuri. Unajua ukimchukia mtu unaweza kujibania baraka zako,” alisema Shamsa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here