21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Shamim Mwasha, mumewe washtakiwa kwa uhujumu uchumi

PATRICIA KIMELEMETA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imempandisha kizimbani mfanyabiashara, Abdul Nsembo maarufu Abdukandida (45) na mke wake Shamim Mwasha (41) kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 232.70.

Washtakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, walisomewa mashtaka hayo mahakamani hapo jana na wakili wa Serikali, Costantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina.

Wakili Kakula alidai kosa lao ni la uhujumu uchumi yenye kesi namba 36/2019 ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kusafirisha dawa za kulevya kinyume na sheria.

Alidai kuwa tukio hilo walilifanya Mei Mosi mwaka huu kwa pamoja wakiwa maeneo ya Mbezi Beach na kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu 232.70, huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Kakula alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Mhina alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa kosa wanaloshtakiwa nalo ni la uhujumu uchumi, hivyo mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na watuhumiwa hawana dhamana.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Hajra Mungula aliuomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi ili hatua nyingine ziweze kuendelea.

Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 27itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles