31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Shambulio la kigaidi laibua mpango wa ‘Nyumba 10’

NA ISIJI DOMINIC

WAKENYA na dunia ilisimama kwa pamoja kulaani kitendo cha ugaidi kilichotokea Januari 15, mwaka huu maeneo ya 14 Riverside Westlands jijini Nairobi ambapo watu 21 walithibitika kupoteza maisha.

Shambulio hilo ambalo lililenga zaidi hoteli ya DusitD2 limetokea takribani miaka sita baada ya tukio kama hilo la kigaidi lililotokea katika maduka ya Westgate jijini Nairobi na kuacha watu 71 wakipoteza maisha.

Katika matukio haya mawili ambayo kundi la kigadi la al-Shabaab limekiri kuhusika, waliokuwa wanafanya mauaji ni watu ambao wamejichanganya na jamii. Rais Uhuru Kenyatta, akihutubia taifa na kudhibitisha kumalizika kwa oparesheni hiyo ambayo magaidi wote waliuwawa na zaidi ya watu 700 kuokolewa, alisema wale wote waliohusika kwa namna moja au nyingine watasakwa, kukamatwa na kuhukumiwa.

Tayari tumeshuhudia maofisa usalama wa vitengo mbalimbali wakiwashikilia watuhumiwa waliohusika na tukio hilo la kigaidi na jambo ambalo linawashangaza wengi ni namna hata wale wauwaji walivyoweza kujichanganya na jamii.

Kufuatia lile shambulio la maduka ya Westgate, Rais Uhuru kupitia kauli yake ya ‘usalama unaanza na mimi na wewe’, alisisitiza umuhimu wa majirani kutambuana si tu kwa sura mbali shughuli wanazofanya.

Ni kauli ambayo ilibuni mpango wa ‘Nyumba 10’ wenye lengo la kila watu kati ya nyumba 10 kutambuana. Hii inasaidia taarifa kuwafikia polisi, yule ambaye unambaini tabia na shughuli zake hazieleweki.

Mashuhuda katika tukio la DusitD2 walisema nyumba la kifahari walilonunua magaidi haikuonesha dalili kwamba walikuwa watu wenye nia mbaya. Walisema licha ya kuingia na kutoka, walikuwa na tabia ya kuzungumza na kutaniana na walinzi. Hali ilikuwa hivyo hivyo kila walipokuwa wakienda kupata chakula katika mgahawa uliopo DusitD2.

Serikali inapaswa kurudi tena na kuboresha mpango wa ‘Nyumba 10’ ambao unaonekana kufanikiwa zaidi vijijini kuliko mjini. Ikumbukwe pia vitendo hivi vya kigaidi ambavyo maisha ya watu wengi hupotea mbali na kufanyika sana kaunti za Lamu, Mandera na Garissa, miji ambayo imelengwa zaidi ni Nairobi na Mombasa.

“Tusiwaruhusu watu hawa (magaidi) kujificha kati yetu. Nawasisitizia kuwapa taarifa polisi au mamlaka yoyote karibu yako unapomuona mtu ambaye humuelewi au tabia zake ambazo si za kawaida,” alisema Rais Uhuru.

Nao vinara wa upinzani, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka, waliwataka Wakenya kukataa kugawanywa kwa kila namna iwe dini, kabila au siasa ambayo magaidi hutumia kuvuruga amani na kufanya vitendo vyao vya mauaji.

Tukio la DusitD2, ile ya Westgate mwaka 2013 na ulipuaji wa balozi za Marekani jijini Nairobi na Dar es Salaam, umewaacha wengi na maswali kwanini hususani Kenya imekuwa ikilengwa zaidi.

Kaunti za Garissa, Lamu na Mandera ambazo al-Shabaab wamekuwa wakizishambulia zaidi zipo karibu na mpaka wa Somalia. Ikumbukwe pia Kenya ilipeleka jeshi lake nchini Somalia kupambana na magaidi ambao nao wanalipiza kisasi wakitaka Serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake.

Ukaribu wa Kenya na nchi za magharibi hususani Marekani pia inaelezwa ni sababu nyingine ya nchi hiyo jirani kushambuliwa huku magaidi wakiamini Marekani wanatumia Jeshi la Kenya kuwashambulia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles