25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

Shahidi akwamisha usikilizwaji kesi Lucky Vincent

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

SHAHIDI wa tano katika kesi ya makosa ya usalama barabarani inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni yaShule ya Msingi Lucky Vincent, amekwamisha kuendelea kusikilizwa kwa shaurihilo baada ya kushindwa kufika mahakamani hapo jana.

Mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha jana, Wakili wa Serikali, Khalili Nuda, alimtaja shahidi huyo kuwa ni Meneja wa Shirika la Bima la Zanzibar Kanda ya Kaskazini, MohamedMatumula.

Alidai mahakamani hapo, licha ya shahidi huyo kupewa hati ya wito wa mahakamani hapo, alidai kuwa amesafiri kikazi yuko jijini Dodoma kwenye vikao.

“Tumefanya jitihada zakumtafuta shahidi huyo ila ameomba udhuru tena kuwa ameitwa Dodoma kwenye vikaona kuomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya shahidi huyo kuja kufanyiwa mahojiano na wakili wa utetezi,” alidai.

Hii ni mara ya pili kwa shahidi huyo kushindwa kufika mahakamani hapo ambapo awali Novemba 22, mwakahuu, alidaiwa yuko jijini Dar es Salaam kikazi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Niku Mwakatobe, alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 12, mwaka 2019.

Novemba mosi mwaka huu, Mahakama hiyo iliagiza shahidi huyo ambaye alishatoa ushahidi wake mahakamani hapo Mei 9 mwaka huu, kuitwa tena na kuhojiwa kuhusu ushahidi wake.

Kuitwa kwa shahidi huyo kunatokana na ombi lililowasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa utetezi, Method Kimomogoro, kufuatia marekebisho ya hati ya mashtaka yaliyofanywa na upande wa Jamhuri na Mahakama hiyo kuamuru kuitwa tena kwa shahidi huyo ili ahojiwe tena.

Katika kesi hiyo, namba 78 ya mwaka jana, Mkurugenzi huyo, Innocent Moshi na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule, Longino Nkana, wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwemo kusafirisha wanafunzi bilavibali maalumu.

Baada ya kufanya marekebisho ya hati hiyo ya mashtaka Novemba mosi mwaka huu, upande wa Jamhuri uliielezaMahakama hiyo kuwa wana kusudio la kufunga ushahidi baada ya kuwa na mashahidisita.

Akiwasilisha ushahidi wake, Mei 9, mwaka huu, Matumula alidai gari hilo lililokuwa na namba za usajili T 871 BYS aina ya Mitsubishi Rossa, halikuwa na bima halali na kuwa bima halali ya gari hilo ilikuwa imekatwa na mmiliki wa awali wa gari hilo katika Shirika hilo ambaye ni Swalehe Kiluvia, ambaye alikata kwa ajili ya matumizi ya biashara.

Moshi anakabiliwa na mashtaka manne ikiwemo kufanya biashara ya usafirishaji abiria bila kuwa na leseni, kuruhusugari kutumika bila kuwa na bima, kushindwa kuingia mkataba na mwajiriwa wake nakuzidisha abiria 13 huku Nkana akikabiliwa na shtaka moja ambalo ni kuzidishaabiria katika chombo cha usafiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles