27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Shahidi abanwa mshtakiwa kutoa rushwa kwa waziri

KulwaMzee, Dar es Salaam

Shahidi wa nne wa Jamhuri, Kamishna Msaidizi wa Ardhi, Mathew Nhonge katika kesi dhidi ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group Company Ltd na Kiluwa Free Processing Zone, Mohamed Kiluwa (50), amebanwa kwanini mshtakiwa atoe rushwa kwa waziri wakati viwanja alipata kihalali.

Mshtakiwa huyo anayedaiwa kutoa rushwa Shmilioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipata hati za viwanja 70 kihalali.

Hayo yamedaiwa leo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mbele ya Hakimu Mkazi,  Samweli Obas, wakati shahidi huyo akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo.

Akitoa ushahidi Mathew amedai Kampuni ya Kilua iliomba kumiliki ardhi maeneo ya Kikongo Kibaha, hati za kumiliki viwanja 73 zilimfikia kwa ajili ya kuzisaini.

Wakili wa utetezi alihoji kama mshtakiwa alitoa rushwa katika halmashauri na kwa kamishna ili kupata hizo hati lakini shahidi alikana kwa kusema kwamba hajawahi kusikia wala kupokea hela kutoka kwake.

Alidai kati ya hati hizo zilisainiwa 70 kisha kupelekwa kwa msajili ya hati na hati tatu hazikusainiwa kwa sababu kulikuwa na upungufu.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Julai 16,  mwaka huu kati ya saa sita na saa nane mchana akiwa Mkurugenzi wa kampuni hizo mbili, alitoa rushwa ya Dola za Marekani 40,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 90 kwa Waziri Lukuvi.

Mshtakiwa anadaiwa kutoa  fedha hizo kwa lengo la kwamba asiwasilishehati ya umiliki wa kiwanja namba 57 Kitalu B Kikongo na D Disunyura kilichopo eneo la viwanda lililopo Kibaha mkoani Pwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles