24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Shabiki wa A$AP Rocky atishia kulipua ubalozi

WASHINGTON D.C, MAREKANI

SHABIKI mmoja wa msanii A$AP Rocky jijini Washington D.C,nchini Marekani, amekamatwa na polisi baada ya kutishia kulipua ubalozi wa Sweden nchini humo kutokana na msanii huyo kuendelea kusota mahabusu.

Mapema mwezi huu msanii huyo alikuwa nchini Sweden kwa ajili ya ziara ya muziki, lakini kabla ya kufanya tamasha alijikuta akipelekwa mahabusu kutokana na kudaiwa kumpiga shabiki wake.

Tangu hapo hadi sasa msanii huyo bado anashikiliwa na jeshi la polisi, hivyo mashabiki wa muziki na wadau mbalimbali wameshangaa kuona bado anaendelea kusota ndani japokuwa rais wa Marekani, Donald Trump kuingilia kati.

Kwa mujibu wa TMZ, shabiki anayejulikana kwa jina la Rebecca Kanter, alionekana karibu na ubalozi huo huku akiwa na chupa yenye kimiminika ndani huku akisema atalipua endapo watachelewa kumuachia rapa huyo, hivyo shabiki huyo amekamatwa kutokana na kauli hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles