22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Shabiki Man U alamba donge nono SportPesa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

ABDULAZIZ Ibrahim amekabidhiwa Sh521,471,360 na kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa baada ya kubashiri kwa usahihi Jackpot ya mechi 13.

Akizungumza wakati wa makabidhiano katika ofisi za SportPesa jijini Dar es Salaam, Abdulaziz mwenye umri wa miaka 24 na mkazi wa Tabora-Sikonge, alieleza furaha yake baada ya kujaribu mara kadhaa bila mafanikio.

Mshindi wa Jackpot ya SportPesa, Abdulazizi Mussa Ibrahim (kulia), akikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 521,471,360 na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas, baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 13 za Jackpot.

Shabiki huyo wa Yanga na Manchester United alisema siku aliyoshinda, aliweka mikeka 10 ya Sh2,000 kila mmoja na mkeka namba saba ndiyo iliyompa ushindi baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote.

“Siku niliyoweka mikeka yangu niliikosesha ushindi Man U ambayo ilikuwa inacheza na Leicester City kupelekea kufanikisha vizuri ushindi wangu,” alisema Abdulaziz ambaye pia ni mwajiriwa wa duka la dawa na maabara.

Mechi ambayo Abdulaziz ‘aliinyonga’ timu yake ya Man U ni ile ya Kombe la FA robo fainali walipopoteza 3-1 kwa Leicester City.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas, alisema mshindi alipatikana Machi 23 mwaka huu lakini ilibidi wasubiri kipindi cha maombolezo kimalizike ndipo waendelee na sherehe ya kumkabidhi Abdulaziz donge lake nono.

Mshindi wa Jackpot ya SportPesa, Abdulazizi Mussa Ibrahim (wa tatu kutoka kulia), akikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 521,471,360 na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas (kushoto), na wachezaji ya klabu ya Simba na Yanga baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 13 za Jackpot.

“Katika ushindi wake Abdulaziz ameweza kubaki na shilingi 417,177,488 huku akitoa shilingi 104,293,872 kama malipo ya kodi ya zuio,” alisema Tarimba na kuongeza kuwa lengo lao ni kuendelea kuwainua vijana wa Kitanzania na kuhakikisha wanabadilisha maisha yao.

“Kila siku tunaendelea kuwa wabunifu ili kuhakikisha tunaboresha huduma na kuwafanya wateja wetu wazidi kufurahia kucheza na SportPesa.”

Tarimba alisema hivi sasa Jackpot yao imepanda upya na kufikia kiasi cha shilingi 218,361,140 ambapo kwa atakayebashiri kwa usahihi mechi 13 ataibuka mshindi na kwa watakaobarishi kwa usahihi kuanzia mechi 10 hadi 12 watapata bonasi ya wiki.

“Endapo Jackpot haitopata mshindi kwa wiki hiyo huongezwa mpaka pale mshindi atakapopatikana,” alisema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles