SHABIKI AVURUGA TAMASHA LA JAY-Z, BEYONCE JUKWAANI

0
994

NEW YORK, Marekani


TAMASHA la wanamuziki mahiri,  Beyonce na mumewe Jay-Z, limemalizika kwa vurugu baada ya kijana mmoja kuvamia jukwaani wakati mastaa hao wakitumbuiza.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki mjini Atlanta nchini Marekani wakati vinara hao wakitumbuiza, ambapo ghafla kijana huyo akapanda jukwaani na kuanza kuwavuruga wanenguaji, hali ambayo ilisababisha tafrani.

Kwa mujibu wa picha za video zilizokuwa zikirekodi tamasha hilo, zinamwonesha kijana huyo akikatiza jukwaani, baada ya kuchomoka kutoka kwa watazamaji kwa kasi na kujikuta akifukuzwa na wanenguaji.

Picha hizo za video zinaonesha kuwa wakati tukio hilo linatokea, baadhi ya wasanii wengine waliokuwa jukwaa la juu walikuwa hawafahamu kinachoendelea, kwani wanaonekana wakiendelea kutumbuiza.

Picha nyingine za video zilizorushwa na mashabiki ambao wanahoji walinzi walikuwa wapi wakati huo, zinawaonesha wakiwa wamemdhibiti mvamiaji huyo baada ya kufanikiwa kumtia mikononi.

“Siwezi kuamini shabiki anaweza kukatiza jukwaani kama hivi,” aliandika mmoja wa mashabiki kupitia ukurasa wake wa Twitter kabla ya kuhoji mahali walipokuwa walinzi hao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here