26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Sh milioni 930 kuboresha Bandari ya Kagunga

ESTHER MBUSSI- KIGOMA

JUMLA ya Sh milioni zimetengwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kwa ujenzi wa barabara na kulipa fidia wakazi katika Bandari ya Kagunga mkoani hapa, inayounganisha mpaka wa Burundi na Tanzania.

Pia imetoa Sh milioni 190 kwa ujenzi wa soko la kisasa lililopo karibu na bandari hiyo ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 45.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma jana,  Meneja wa Bandari ya Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, alisema hatua hiyo inatokana na barabara ya lami kuishia katika mpaka wa Burundi huku njia ya kuifikia bandari hiyo ambayo ni mita 700 ikiwa ya vumbi.

“Katika bandari hii kuna barabara ya kiwango cha lami lakini imeishia katika mpaka wa Burundi hivyo barabara ya kuingia bandarini haijaunganishwa hivyo TPA imetenga fedha hizo kwa ajili ya kulipa fidia za wakazi na kujenga barabara za kiwango cha changarawe.

“Lakini pia tuna lengo la kushirikiana na Halmashuari ya wilaya hii kufanya mradi wa ujenzi wa soko ni kufungua fursa za kibiashara katika bandari hiyo inayounganisha nchi za Tanzania, Burundi na Congo.

“Pamoja na mambo mengine, bandari hii ni ya kimkakati hivyo ni muhimu kuwa na mazingira mazuri kama miundombuni imara ili kuunganisha nchi hizo tatu kibishara,” alisema.

Kuhusu biashara alisema bidhaa nyingi zinazoletwa na meli bandarini hapo zinatoka  katika nchi za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Aidha, akizungumzia miradi inayoendelea bandarini hapo alisema tayari ujenzi wa gati litakalosaidia meli kutia nanga umekamilika, majengo ya ofisi, nyumba za wafanyakazi, jengo la abiria, ghala na mengine.

“Kukamilika kwa miradi hi, kutawezesha bandari  kupata mapato ya kutosha,” alisema.

Naye Kaimu Mhandisi wa Bandari ya Ziwa TanganyikaTPA, Injinia Nyakato Mwamnana, alisema ujenzi wa gati hilo litakalodumu kwa zaidi ya miaka 50, umegharimu Sh bilioni 3.3 ambapo ulianza Agosti mwaka 2015.

“Uwepo wa gati hili utasaidia kuhudumia shehena katika nchi za Burundi, Congo na Tanzania na utaziunganisha nchi hizo katika kukuza uchumi.

“Pia gati hili lina ukubwa wa mita 20 na inaweza kuhudumia meli yenye urefu mita 72 wa kina cha mita tano.

Akizungumzia ujenzi wa soko hilo, Kidawa Bakari ambaye anafanya biashara ya genge, alisema utawasaidia kukuza biashara zao kutokana na mwingiliano wa wafanyabiashara wengine kutoka Burundi.

“Soko hili likiisha tutafanya biashara hasa siku ya soko, kwani kwa sasa tumekuwa tukipata tabu hasa wakati wa mvua kwani hakuna mahali pa kujikinga,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles