29.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Sh bilioni nane kutumika kupanga upya Jiji la Mwanza

NA BENJAMIN MASESE, MWANZA

SERIKALI inakusudia kutumia Sh bilioni nane katika mpango wake wa kulipanga upya Jiji la Mwanza kwa kuainisha sehemu za makazi, viwanda, biashara na huduma za kijamii.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mkurugenzi Msaidizi wa Mpango Mkakati wa Kuyapanga Majiji kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mahenge Amulike, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau na viongozi wa Serikali wa sekta zote wa kupokea maoni na mapendekezo ya kuainisha maeneo hayo.
Pia aliwataka wakazi wa Mwanza na Arusha kutambua hakuna haja ya kumiliki eneo kubwa la ardhi kwa ajili ya kujenga nyumba nyingi, badala yake wanapaswa kumiliki eneo dogo ili kujenga ghorofa.

Alisema Serikali imeamua kuainisha maeneo ya majiji hayo kwa sababu ya ardhi kutoongezeka, huku watu wakiongezeka kwa kasi, hivyo ni lazima maeneo yakapangwa katika utaratibu unaotakiwa, ikiwa ni kuepusha majanga yanayotokana na watu kuishi katika maeneo hatarishi bila wao kujua.

Alisema tatizo kubwa lilipo kwa Watanzania ni kutaka kumiliki eneo kubwa la kujenga nyumba, kitendo kinachosababisha watu wengine kukosa ardhi na kukosekana sehemu ya kuweka huduma za kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles