29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

SETHI WA IPTL APINGA KUENGULIWA UKURUGENZI

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


SIKU moja baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), kutangaza kumwondoa kwenye ukurugenzi, aliyekuwa Mwenyekiti wao, Harbinder Sing Sethi, hatimaye kigogo huyo amepinga uamuzi huo.

Sethi amesema bado yeye ni kiongozi halali na hatambui mabadiliko ya aina yoyote.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na mwanasheria wake, Hajra Mungula, imesema Sethi amesikitishwa na taarifa ya mabadiliko kwa uongozi wa kampuni hiyo na kushangazwa na mtu aliyejiita mwenyekiti wa IPTL.

Hajra alisema Sethi ameagiza wanasheria wake kuchukua hatua za haraka za kisheria kwani hana taarifa zozote juu ya mabadiliko hayo, akitaka umma upuuze taarifa hizo kwani hazitokani na mamlaka halali za kisheria za IPTL.

“Hivi karibuni mmesikia imeripotiwa katika vyombo vya habari kwamba kampuni inayomilikiwa na Harbinder Sing Sethi imebadilisha uongozi katika ngazi za Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi Mtendaji ambapo taarifa iliyosambazwa na anayejiita mwenyekiti wa bodi mpya, Ambroce Brixio Lugenge imemtaja yeye kuwa na cheo hicho na Joseph Makandege kuwa mkurugenzi wake ambaye kwa miezi kadhaa sasa hajawahi kuonana nae, ikiwemo hata kutofika mahakamani siku ambazo kesi imekuwa ikitajwa.

“Taarifa hizo zimemfikia kwa masikitiko makubwa sana mwenyekiti halali na mmiliki wa kampuni hii ya kuzalisha umeme ya IPTL ambayo kimsingi inamilikiwa na kampuni anayoimiliki ya Pan Africa Power Solutions (PAP).

“Pamoja na kuagiza wanasheria wake kuchukua hatua za haraka za kisheria, Mwenyekiti Sethi pia hana taarifa zozote juu ya mabadiliko hayo na hivyo anapenda kuutaarifu umma kupitia sisi kwamba wazipuuze taarifa hizo kwa kuwa hazitokani na mamlaka halali za kisheria za kampuni hiyo,” alisema Hajra katika taarifa hiyo.

Alisema pamoja na kwamba Sethi bado yuko mahabusu akituhumiwa mashtaka kadhaa ya jinai, hiyo haiondoi ukweli kuwa IPTL ni kampuni binafsi yenye wamiliki halali wenye hisa halali na wala si NGO ambayo mtu yeyote anaweza kutangaza mapinduzi ya kiuongozi wakati wowote.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles